Aliyekuwa Waziri Wa Maliasili na Utalii
Mhe.Khamis Kigwangala.
MDHIBITI
na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), Charles Kichere amesema
Ripoti imemuweka matatani aliyekuwa Waziri Wa Maliasili na Utalii, Khamis Kigwangala alivyotumia madaraka yake vibaya na kuisababishia hasara Serikali katika kampeni yake ya kuhamasisha upandaji Mlima Kilimanjaro.
Mbali na taarifa hiyo amegusia sekta za kiserikali na binafsi mbalimbali zilizobainika kuwa kinyume na matumizi ya Serikali
Akitoa
muhtasari wa ripoti hiyo jijini Dodoma, jana CAG Charles Kichere
amesema, katika tamasha la Urithi Festival lililofanyika mwaka 2019,
kulikuwa na viashiria vya ubadhirifu wa fedha kutokana na kanuni
mbalimbali kukiukwa.
Tamasha hilo lilifanyika chini ya uongozi wa Dk. Kigwangalla wakati akiwa Waziri wa Maliasili na Utalii.
CAG
Kichere amesema, fedha zilizotumika kufanikisha tamasha hilo, hazikuwa
katika bajeti ya wizara hiyo, wala hakukuwa na mpango ulioidhinishwa wa
utekelezaji wake.
Amesema,
kutokana na fedha hizo kuwa nje ya bajeti, wizara hiyo ilichangisha
kiasi cha shilingi bilioni moja kutoka katika wakala zake nne ambazo ni
Shirika la Hifadhi za Taifa (TANAPA), Wakala wa Huduma za Misitu (TFS),
Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro (NCAA) na Mamlaka ya Usimamizi
wanyapori Tanzania (TAWA) huku wizara hiyo ikichangia shilingi milion 299
na kiasi cha bilioni 1.57 zilipatikana na hazikuwa kwenye bajeti za
wizara na taasisi husika.
Pia
Kichere amesema kuwa milioni 487 zilipelekwa kwenye taasisi saba kwa
ajili ya utekelezaji wa tamasha la urithi ambapo hakukuwa na nyaraka
zilizowasilishwa kwa ajili ya ukaguzi ili kudhibiti matumizi hayo ambapo
pia Shilingi milioni 585.52 yaliyolipwa na mhasibu wa mfuko wa tozo ya
maendeleo ya utalii bila ya kuwa na nyaraka toshelezi.
"Mnamo Septemba 28, 2019 aliyekuwa waziri wa maliasili na utalii alizindua
shindano lililoitwa Kigwangala Kill Challenge lililojenga kuhamasisha
watu kupanda mlima Kilimanjaro ambapo lilitumia shilingi milioni 172
zilizotolewa na NCAA huku shilingi milioni 114.50 na TANAPA milioni
57.50 bila kuwa katika bajeti zao za mwaka wa fedha 2019/20.
Aidha
kwa upande wake Mwenyekiti wa Kamati ya hesabu za Serikali Japhet
Hasunga na Mwenyekiti wa Kamati ya Hesabu za Serikali za Mitaa naye kwa
pamoja wameipongeza ripoti ya CAG huku akisema kama Bunge wataifanyia
kazi katika kusimamia mali za Serikali kutokana na ripoti hiyo.
No comments:
Post a Comment