Baadhi ya wabunge na wanaharakati wakupinga ukatili wa kijinsia.
NA HAMIDA RAMADHANI, DODOMA
MRATIBU
wa Mtandao wa jinsia Tanzania ,Tanzania Gender Networking Programme
(TGNP) Zainabu Mmari amesema kuwa tangu kuanzishwa kwa harakati za
ukombozi wa wanawake nchini Wanawake wengi wameweza kujitambua,kujua
haki zao na kutetea mahitaji yao ya Msingi katika ngazi husikia.
Akiongea
na waandishi wa habari Jijini Dodoma mara baada ya kumalizika kwa
mafunzo waliopatiwa wabunge wanawake juu ya masuala mazima yanayohusu
ukatili Zainabu amesema wao kama TGNP muda wa miaka mitano nyuma
wameamua kuwekeza nguvu kubwa katika ngazi ya Jamii.
"
Sio kwamba tumeacha kujikita katika ngazi ya serikali Kuu hapana
tumeamua kufanya hivyo ili tuweze kuwafikia wananchi wengi ambao ndio
wameonekana ndio wenye uhitaji," amesema Zainabu.
Amesema
kuwa wamefanya kazi katika maeneo ya upatikanaji wa kijamii ikiwemo
Afya, Elimu Maji na sasa wamejikita katika eneo la Kilimo ambapo ndipo
kumeonekana kunakundi kubwa la wanawake wengi zaidi ya asilimia 55
wamejiajiri
kwa kutumia Kilimo.
Pia
amesema wameanza kuangazi kwa wanawake ambao ni wachimbaji wadogo
wadogo na kuna maeneo ambayo wanafanyia kazi kama vile Wilaya ya
Morogoro vijijini ,Wilaya ya Mbeya Vijijini,Wilaya ya Shinyanga
Kishapu,Tarime na Kasulu.
Amesema
wameweza kujenga nguvu kubwa ndani ya jamii katika kumkomboa mwanamke
kimapinduzi na kuaanzisha vituo vya taarifa na maarifa ambavyo
vinaendeshwa na wanawake waliowezeshwa na wanaotambua haki
zao,wanaotetea masuala ya kijinsia,wanauwezo wa kufuatilia ngazi tofauti
tofauti za Serikali kuanzia ngazi ya kijiji ,Kata,hadi Halmashauri na
kuona ni namna gani masuala hayo yanaweza kuingizwa kwenye Mipango na
bajeti za Serikali.
" Kwa
Kiasi kikubwa tumefanikiwa mpaka kufikia kwa baadhi ya Halmashauri
wanapokuwa na vikao vyao vya kupitisha bajeti wanatualika hivyo vituo
vya Taarifa na Maarifa ngazi ya Jamii kwa ajili ya kuangalia na kutoa
mapendekezo yao ili yaweze kuingizwa kwenye bajeti za Halmashauri,"
amesema Zainabu.
ATHARI ZA VITENDO VYA UKATILI KWA WAWAKE NA WATOTO.
Amesema
changamoto ni kubwa kwani mwanamke au mtoto wa kike au mtu yoyote
katika jamii anapofanyiwa vitendo Vya ukatili kwanza kabisa
vinamuondolea kujiamini hata maendeleo yake hata ushiriki kwenye jamii
unapungua.
" Na
imeonekana wanawake wengi au watoto wa kike wanaofanyiwa ukatili
kwasabau ya ukosefu wa kipato au uchumi mdogo kuanzia ngazi ya Jamii,
familia na wakati mwingine anaweza kuona viashiria vya ukatili lakini
anashindwa kuondoka kwasabau ya hofu ya kujifunza mwenyewe na familia
kwa Jumla.
Amesema
vitendo hivyo vimewaathiri Sana kwani utakuta mwanamke anafikia hatua ya
kijifungia ndani kwasabau ya kunyooshewa vidole na Jamii vitendo hivyo
vinawaharibu wanawake kisaikolojia.
Naye
Mussa Jonasi ambaye anafanyia kazi na Shirika la TGNP Mkoani Shinyanga
Amesema mfumo dume Umasikini na imani za kishirikiana,mila kandamizi
ndio chanzo cha vitendo Vya ukatili katika ngazi ya jamii hadi ngazi ya
familia.
No comments:
Post a Comment