HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

April 16, 2021

Waandishi wa habari wafundwa

 


Aliyekuwa Msemaji Mkuu wa Serikali Dkt. Hassan Abbasi leo Aprili 16, 2021 amekabidhi ofisi ya Mkurugenzi wa Idara ya Habari Maelezo ambayo pia ni  Msemaji Mkuu wa Serikali kwa Bwana  Gerson Partinus Msigwa ambaye ameteuliwa hivi karibuni  na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Samia Suluhu Hassan kuwa Mkurugenzi wa Idara hiyo na  Msemaji Mkuu wa Serikali. Makabidhiano hayo yamefanyika katika Ukumbi wa Idara ya Habari Maelezo jijini Dodoma. (Picha na Maelezo).

 

NA HAMIDA RAMADHANI, DODOMA

 

MSEMAJI  Mkuu wa Serikali  na Mkurugenzi wa Idara ya Habari Maelezo Gerson Msigwa  amewataka waandishi wa habari hapa nchini kuzingatia Sheria, Kanuni, taratibu ,Miongozo na Taaluma ya uandishi wa habari Katika utekelezaji wa majukumu yao.


Msigwa ametoa kauli hiyo leo jijini Dodoma mara baada ya kukabidhiwa ofisi na aliyekuwa Msemaji Mkuu wa Serikali  na Mkurugenzi wa Idara hiyo Dkt . Hasan Abbasi aliye hudumu katika nafasi hiyo katika kipindi cha miaka minne na miezi minane.


"Wakati huo huo amesema atasikitika kuona kuwa Waandishi wa Habari na Vyombo vya habari vinatumika kwaajili ya kuibomoa nchi,serikali na kurudisha nyuma juhudi zilizofanywa na watanzania tangu Tanzania ipate uhuru", amesema Msigwa.


Katika hatua  nyingine Msigwa amesema haikubaliki kwa mwandishi wa habari kunyanyaswa kwa namna yeyote ile pindi anapokwenda kutekeleza majukumu yake ya kazi.


Kwa upande wa aliyekuwa Msemaji Mkuu wa serikali Dkt Abas ambaye ni Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari,Utamaduni ,Sanaa na Michezo amemshukuru Hayati Dkt John Pombe Magufuli kwa nafasi aliyo mpa wakati ule na kumshukuru Rais Samiah Suluhu Hasan kwa kuendelea kumuamini katika kuitumikia nchi.

No comments:

Post a Comment

Pages