Kituo cha Uwekezaji nchini (TIC) kimesema katika
kipindi cha mwezi januari hadi machi mwaka huu, kimefanikiwa kusajili
jumla ya miradi mipya 51 yenye thamani ya dola za kimarekani 451 milioni
huku kikibainisha sekta ya viwanda kuongoza katika miradi hiyo kwa kuwa
na miradi 30 sawa na asilimia 59 ya miradi yote.
Hayo
yamesemwa hii leo jijini Dar es Salaam na Mkurugenzi Mtendaji wa Kituo
hicho, daktari Maduhu Kazi wakati wa utoaji wa taarifa ya robo tatu mwaka
2020/2021 kwa waandishi wa habari.
Daktari
Kazi amesema miradi hiyo inatarajia kuzalisha ajira mpya 4,272 sawa na
ongezeko la asilimia 3.5 ukilinganisha na kipindi kama hicho mwaka jana
ambapo miradi 54 ilisajiliwa ambyo ilitarajiwa kuwekeza mtaji wa dola za
kimarekani 283 milioni iliyozalisha ajira 4,127
"sekta
iliyoongoza kwa uzalishaji wa ajira mpya ni utalii ambapo inategemea
kuzalisha ajira 572 sawa na asilimia 13.4 ya ajira zote,"amesema dkt
Kazi.
Amebainisha kuwa
kati ya miradi 51 iliyosajiliwa mwaka huu miradi 13 sawa na asilimia 25
ni miradi ya wawekezaji wa ndani,miradi 26 sawa na asilimia 51 ni miradi
ya wawekezaji wa kigeni,na kusisitiza miradi 12 sawa na asilimia 24 ni
miradi ya ubia kati ya watanzania na wageni.
Aidha
amesema TIC kinatunza kumbukumbu za miradi ya uwekezaji iliyosajiliwa
hivyo wawekezaji ambao wamewekeza nchini bila kupitia kituo hicho hawako
katika takwimu hizo badala yake wawekezaji wengine husajiliwa na
EPZA,Tume ya madini na wengne huwekeza bila kupitia katika taasisi hizo.
Ameongeza
kuwa katika kuendelea kuboresha uwekezaji nchini kituo hicho
kimejiwekea mikakati mbalimbali ikiwemo kuendelea kuboresha mfumo wa
kusajili miradi unaotumiwa na kituo hicho,kuunganisha mfumo wa kusajili
miradi (TIW)unaotumika na TIC na mifumo mingine inayohudumia wawekezaji
nchini.
Mikakati mingine
ni kuhamasisha zaidi uwekezaji kwa wazawa na ubia,kufuatilia kwa karibu
wawekezaji kwa lengo la kung'amua changamoto zinazojitokeza katika
utekelezaji wa miradi yao,pamoja na kuboresha zaidi matumizi ya tehama
katika shughuli zote za kunadi na kuhumia wawekezaji.
Dkt.
Kazi alisema kituo hicho kinaendelea kuwakaribisha wawekezaji kuja
kuwekeza nchini kwani mazingira ya uwekezaji yameboreshwa.
No comments:
Post a Comment