Meneja Mawasiliamo na Elimu kwa Umma wa TMDA Gaudensia Simwanza akizungumza na waandishi wa habari.
NA ASHA MWAKYONDE
MAMLAKA ya Dawa na Vifaa Tiba Tanzania (TMDA),inatarajia kuwajengea uwezo Wachunguzi wa dawa za kuua viini vya bakteria (Vipukusi), kwa lengo la kuwafanya kuwa wabobezi katika Maabara ya Kanda ya Ziwa.
Maabara hiyo ya Kanda ya Ziwa ipo kwenye mpango kuwanywa
kuwa maabara kubwa ya kisasa na bobezi ya kupima Vipukusi katika Afrika na nchi za Kusini mwa Afrika (SADC).
Akizungumza na mwandishi wa habari hizi jijini Dar es Salaam jana Meneja Mawasiliamo na Elimu kwa Umma wa mamlaka hiyo Gaudensia Simwanza amesema Maabara zote duniani lazima ziwangee uwezo Wachunguzi wao ili waweze kufanya vizuri.
Meneja huyo amesema lengo la kuwa jengea uwezo Wachunguzi hao ni kuandana na Sayansi na teknolojia ya vifaa wanavyovitumia.
Amesema kuwa idadi ya Wachunguzi waliopo ambao watakao jengewa uwezo itawekwa kulingana na mpango ulipo wa Maabara hiyo.
Simwanza amesema Maabara hiyo ya Kanda ya Ziwa imekidhi vigezo elekezi vya Shirika la Afya Duniani (WHO), ambapo inatoa majibu sahihi yanayokubalika ya uchunguzi wa Sampuli za Vipukusi.
" Ili maabara itoe majibu yasiyo na shaka lazima iwe imekidhi vigezo elekezi vya Shirika la Afya Duniani, Maabara hii imekidhi " amesema Simwanza.
Ameongeza kuwa Maabara hiyo tayari imeshapokea vipimo vya Sampuli zilizochungunzwa nchini Ujerumani na Afrika Kusini ambapo baada ya kupima majibu yakaonesha kutofautiana.
Meneja huyo amesema baada ya Sampuli hizo kupimwa katika Maabara ya TMDA majibu yakawa suluhisho.
No comments:
Post a Comment