HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

April 22, 2021

BENKI YA EQUITY TANZANIA YAJA NA MARA TATU ZAIDI NA JIJENGE AKAUNTI

Mkuu wa Masoko na Mahusiano wa Benki ya Equity Tanzania, Godwin Semunyu, akizungumza wakati wa uzinduzi wa huduma mpya ya Mara Tatu Zaidi na Jijenge Akaunti uliofanyika jijini Dar es Salaam leo Aprili 22, 2021.

Baadhi ya mameneja wa matawi ya Equity Bank Tanzania.
Baadhi ya mameneja wa matawi ya Benki ya Equity Tanzania.


Mkuu wa Kitengo cha Biashara Benki ya Equity Tanzania, Isabela Maganga (katikati), akizungumza wakati wa uzinduzi wa huduma mpya ya Mara Tatu Zaidi na Jijenge Akaunti. Kushoto ni Mkuu wa Masoko na Mahusiano Equity Bank Tanzania, Godwin Semunyu na kulia ni Meneja Mahusiano Kitengo cha Biashara Equity Tanzania, Happiness Munisi.

 

Equity Bank (T) Equity Bank (T) leo imenzidua rasmi akaunti maalum ya utunzaji fedha kwa kujiwekea kidogo kidogo ili kufikia malengo ijulikanayo kama “Jijenge Akaunti”.

 

Akaunti ya Jijenge ni mpango wa kujiwekea akiba (savings plan) wenye lengo la kuboresha maisha ya watanzania kwa kuwapa fursa yakujiwekea akiba

Kadri wanavyopata ili kufanikisha mipango yao ya maisha ikiwemo kujenga nyumba, kununua viwanja, kulipa karo na mengineyo.

 

Akizungumza katika hafla ya uzunduzi wa akaunti hiyo jijini Dar es Salaam, Mkuu wa Kitengo cha Biashara wa Benki ya Equity (T) Isabella Maganga amesema kuwa Jijenge akaunti ni suluhisho rasmi la kujiwekea akiba na kufikia malengo.

 

 “Kupitia akaunti hii ya Jijenge mteja anapata nafasi ya kufikia mipango yake ya muda mrefu au mfupi kwa kujiwekea akiba taratibu na hatimaye kufikia malengo. Jijenge akaunti ni daraja la kufikia ndoto za Maisha kupitia kujiwekea akiba. Kubwa Zaidi ni kuwa ukiweka akiba kwa kipindi cha miezi sita na kuendelea, unaweza kukopa mpaka mara tatu ya fedha ulizojiwekea” alisema.

 

 Akizungumza kuhusu taratibu za ufunguaji na uendeshaji wa akaunti hiyo ya Jijenge; Bi.Masanja alisema “Ili kufungua akaunti ya Jijenge, mteja anahitaji kuwa na kitambulisho cha NIDA pekee,  na kianzio ni shilingi elfu kumi tu. Kama ilivyo kwa akunti zetu zingine, Jijenge akaunti pia haina makato yoyote ya mwezi na inajipatia riba nzuri na endelevu.

 

Pia tumeweka urahisi wa kujiwekea akiba kwa kuwapa wateja wetu uwezo kutuma pesa kwenye akaunti zao za “Jijenge” kwa kutumia huduma yetu ya Simu za mikononi “Eazzy Banking” huduma kupitia mtandao wa intanenti yaani “Eazzynet” au kwa kutumia utaratibu maalum kuhamisha fedha yaani Standing Order”alisema.

No comments:

Post a Comment

Pages