NA HAMIDA RAMADHANI, DODOMA
NAIBU
Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi (Sekta ya Uchukuzi) Mwita Waitara ameagiza
wakala wa Ufundi na Umeme nchini TEMESA kuhakikisha wanafanya kazi kwa
faida itakayowawezesha kutoa gawio serikalini bila kushinikizwa.
Naibu
Waziriaziri Waitara ametoa agizo hilo jijini Dodoma wakati akizungumza
na menejimenti ya TEMESA mara baada ya kutembelea na kukagua karakana
ambapo amesema ili kuifanya serikali iwe na nguvu ni lazima Taasisi zake
zijiendeshe kwa faida.
Hata
hivyo amewataka wakala hao kuhakikisha kuwa magari na mitambo ya
serikali inayohitaji matengenezo katika karakana za TEMESA kote nchini
yanashughulikiwa kwa haraka.
Pia amewataka kupunguza bei ya utungenezaji wa magari ili Wateja wasikimbie na kwenda kutengeneza kwenye makampuni mengine.
"Naagiza
kwa magari na mitambo iliyotelekezwa katika karakana hii kuyaondoa
haraka ili kuyapa nafasi magari mengine yanayohiji kutengenezwa ndani
ya karakana hii,"amesema Waitara
Hata hivyo amesema TEMESA ni
Taasisi
kubwa na ipo karibu kila Mikoa malalamiko yaliyopo kuwa na bei kubwa
ya matengenezo,magari kuchelewa na Spea kuuzwa kwa bei kubwa na ndio
Maana wataalamu wa TEMESA wanatoka nje na kwenda kufanya mazungumzo na
Wateja ili wawatengenezee kwa bei nafuu.
"Naomba
tuwaangalie wataalamu wetu utakuta mtu ni muajiriwa wa TEMESA halafu
anachukuwa utaalamu wetu anachepuka na kwenda nje kutengeneza magari kwa
kutumia Vifaa vya Taasisi yetu ya TEMESA tabia hii naomba iachwe mara
moja ," amesema
Na
kuongeza kuwa" Tukikugundua tutakushitaki kwa maana unatuibia,kama wewe
una utaalam ,maoni na mawazo yako peleka kwenye vikao vyenu vya
Menejimenti na huyo anaeona huko nje ndio kunamanufaa zaidi atoe maoni
hapa halifu nyie muyachakate maoni hayo na mkubaliane yale mnayoona yana
manufaa kwenu yafanyeni na kama mkishindwa kuna Wizara tutawapa
ushirikiano wa kutosha ili kuboresha Taasisi hii"ameongeza Waziri
Awali
taarifa ya mtendaji mkuu wa wakala wa ufundi na umeme TEMESA Mhandisi
Japhet Maselle imebainisha majukumu ya wakala kwa kipindi cha mwaka wa
fedha unaomalizika ikiwamo utekelezaji wa miradi 35 iliyogawanyika
katika makundi manne ambayo ni ujenzi, ununuzi, ujenzi na ukarabati wa
maegesho ya vivuko pamoja na ujenzi wa karakana.
No comments:
Post a Comment