Waziri
wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Selemani Jafo
leo amekutana na kufanya mazungumzo na Mkuu wa Mkoa waTabora Dk.
Philemon Sengati kwa lengo la kuendeleza agenda ya Uhifadhi wa Mazingira
nchini.
WAZIRI
wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Selemani Jafo
amemuagiza Mkurugenzi wa Manispaa ya Tabora Bosco Ndunguru katika
kipindi cha siku saba kuhakikisha machinjio katika Manispaa yake
yanafanyiwa usafi madhubuti.
Agizo
hilo limetolewa leo na Waziri Jafo mara baada ya kufanya ziara ya
kikazi ya kukagua usimamizi na uzingatiaji wa Sheria ya Mazingira ya
mwaka 2004 Mkoani Tabora. Akiwa katika machinjio hayo Waziri Jafo
ameshuhudia kukithiri kwa uchafu ndani na nje ya jengo hilo jambo ambalo
linahatarisha afya za wakazi wa Tabora.
“Mazingira
ya hapa ni machafu sana, natoa muda wa wiki moja marekebisho yafanyike
na nipate taarifa ya utekelezaji mapema iwezekanavyo pia natoa mwezi
mmoja wa ukarabati wa mfereji wa maji taka” Jafo alisisitiza.
Waziri
Jafo pia ametembea Kampuni ya kuzalisha mkaa mbadala ya “Kuja na
Kushoka” na kutoa rai kwa taasisi za Umma na Binafsi kupunguza matumizi
ya kuni na mkaa na kuhamasisha matumizi ya mkaa mbadala unaozalishwa
kutokana na taka.
“Azma
ya Serikali ni kuhakikisha tunatunza mazingira yetu kwa kupunguza
matumizi ya kuni na mkaa, natoa rai kwa Shule za Binafsi na za Serikali
kununua hizi mashine za kuzalisha mkaa badala ili zitumike kuzalisha
mkaa katika Shule zao pia kama chanzo cha mapato kwa kutengeza mkaa na
kuuzia wengine” Jafo alisisitiza.
Akiwasilisha
taarifa ya Kampuni ya kuzalisha mkaa mbadala Leonard Kushoka amesema,
anatumia teknojia ya kuchakata taka na kuzalisha mkaa mbadala ambao
umekuwa wa manufaa kwa wakazi wa Tabora na Tanzania kwa ujumla kwa kutoa
ajira kwa vijana kunusuru mazingira.
Waziri
Jafo yuko Mkoani Tabora kukagua shughuli za uhifadhi na usimamizi wa
Mazingira ambapo kwa siku ya kwanza amekagua Machinjio ya Manispaa ya
Tabora, Kampuni ya kuzalisha Mkaa mbadala na ukaguzi wa mabwawa ya maji
taka.
No comments:
Post a Comment