HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

May 21, 2021

TMDA Kanda ya Kati yatoa mafunzo kwa wahudumu wa afya

 NA HAMIDA RAMADHANI, DODOMA


MAMLAKA ya Dawa na Vifaa Tiba (TMDA) mkoani Dodoma imetoa mafunzo kwa watoa huduma wa afya kwa lengo la kupunguza matumizi mabaya ya dawa na vifaa tiba huku ikikumbushwa kuendelea kutoa elimu  kwa jamii juu ya matumizi mabaya ya dawa na vifaa tiba.

Akizungumza  katika mafunzo maalum juu ya matumizi ya dawa,  Kaimu katibu Tawala wa mkoa wa Dodoma  Aziza Rajabu Mumba  amesema lengo kubwa la kutoa mafunzo kama hayo  ni kuhakikisha   kupuguza madhara makubwa juu ya athari za dawa kwa watumiaji.

Amesema wamewapa elimu wataalamu hao ambao wako kwenye vituo vya Afya ili waweze kudhibiti madhara ya dawa na Vifaa Tiba yasitokee kwa watumiaji.

Aidha Kaimu katibu tawala huyo wa mkoa  ametoa wito kwa mamlaka ya dawa na vifaa tiba[TMDA]kuendelea kutoa elimu juu ya matumizi sahihi ya dawa na vifaa tiba.

Katika hatua nyingine  amesema  kwa sasa hali sio mbaya  hasa kwenye eneo la madhara ambapo , mambo yamekuwa mazuri, kutokana na elimu kuendelea   kutolewa kila wakati kwa jamii kuhusiana na utumiaji wa dawa na vifaa tiba katika afya ya mwanadamu.

Kwa upande wake kaimu meneja wa mamlaka ya dawa na vifaa tiba[TMDA]   kanda  ya kati  Sonia Henry amesema mafunzo hayo dhima yake kubwa ni kuwakumbusha watoa huduma katika majukumu yao ili kuwa makini katika kutoa huduma inayostahili na kulinda afya ya jamii .

" Tumewapa mafunzo watumishi 30 wa sekta hii ya Afya kutoka Halmashauri zote za Dodoma  lengo likiwa ni kuwajengea uwezo Ili waweze kutoa taarifa zitakazosaidia kupunguza madhara kwa wananchi pindi watumuapo dawa na Vifaa Tiba," amesema 

Mamlaka ya dawa na vifaa tiba ni Taasisi ya serikali iliyopo chini ya wizara ya Afya,Maendeleo ya jamii jinsia wazee na watoto yenye jukumu la kudhibiti ubora,usalama na ufanisi wa dawa,vifaa tiba na vitendanishi ili klinda Afya ya jamii.

No comments:

Post a Comment

Pages