KATIBU
Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi CCM Daniel Chongolo amekutana na waandishi
wa habari huku akitoa maelekezo ya kuondoa vikwazo kwa wananchi katika
Wizara tatu ambazo ni Wizara ya Ardhi Nyumaba na Maendeleo ya Makazi
,Kilimo na Wizara ya Nishati
Akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dodoma Katibu Mkuu huyo amesema hadi
kufikia 2025 Chama Cha Mapinduzi iliahidi kutunza rasilimali za aridhi
ikiwemo kutatua migogoro yote ya ardhi kwani migogoro hiyo ya ardhi
imekuwa ikiwapotezea muda wananchi.
Aidha
amesema Chama Cha Mapinduzi CCM kupitia ilani yake imeielekeza Serikali
kuhakikisha wanatoa hati miliki Katia umiliki wa ardhi na kwakufanya
hivyo utawasaidia wananchi kuwa na Usalama wa maeneo yao.
"
Tumefanya tathimini na tumegundua kwamba mpaka sasa ni wananchi
wachache wanaomiliki ardhi wengi umiliki wa ardhi hawana ," amesema
Chongoro.
Pia amesema kwa
Upande wa uthaminishaji na fidia Wizara utengeneze mfuko wa fidia
utakao leta haki kwa wananchi ambapo amewataka Viongozi wote wa ngazi
zote kuhakikisha wanatatua migogoro ya ardhi katika maeneo yote
yalionekana kuwa na migogoro.
KWA UPANDE WA MABARAZA YA ARDHI
Amesema
Mabaraza ya ardhi yapewe fursa ya kusikiliza nakutatua changamoto
mbalimbali na kuachana na mfumo wa kutoa hukumu na badala yake
wahahikishe wanatoa Suluhu ya migogoro hiyo.
Amesema
katika suala Zima la upimaji wa ardhi wahahikishe wanapima maeneo Ili
kuyapanga na kuondoa ukuaji holela wa miji usiopanga.
"
Pia Wizara ya Aridhi Nyumba na Maendeleo ya makazi kuhakisha
wanaandaa mfumo wa utambuzi kwa maeneo yanayoonekana kukua kwa kasi ili
kuepuka kuwa na miji usiopanga," amesema Chongoro.
WIZARA YA KILIMO
Amesema Kilimo ndio Wizara mama ambayo inabaeba Watu wengi asilimia 70 hadi 80 wapo wananchi wamejikita kwenye Kilimo.
"
Sisi kama Chama tawala tumeiona tuishauri Serikali kwenye bajeti ya
Mwaka 2021/2022 kuweka mkazo Kilimo cha umwagiliaji kwani kwasasa ndio
kimbilio la wengi wakulima kutokana na mvua zisizo eleweka," amesema
Amesema
ili kukuza maeneo ya uzalishaji hekta Milioni 1.2 zitengwe na kila
mwaka watenge maeneo ya umwagiliaji na sikimu za zilizoazishwa kujenga
zikamilike na kwakufanya hivyo wigo wa uzalishaji wa Kilimo utaonekana.
MBEGU
Amesema
changamoto kubwa kwa wakulima ni upatikanaji wa Mbegu bora hivyo Sisi
kama Chama tawala tunaishauri Serikali kuweka bajeti ya Utafiti wa Mbegu
bora Ili kuwapa uhakika wa mazao yao wakulima .
Amezitaka Taasisi zote zinazoshughulika na masuala ya tafiti zijiekekeze na ziwezeshwe Ili ziweze kutoka Mbegu bora.
"
Ili kuwakuza wakulima wetu tunaishauri Serikali kupitia bajeti hii ya
kilimo inayotalijiwa kusomwa hivi karibuni Wizara ya kilimo ijikite
katika kutoa mikopo yenyemanufaa kwa wakulima ikiwemo pembejeo,"
amesema.
WIZARA YA NISHATI
Amesema
kupitia bajeti ya mwaka 2021/2022 Chama Cha Mapinduzi CCM kinaelekeza
yafuatayo kuweka kipaumbele katika upatikanaji wa umeme sehemu zote.
Pia
amesema Chama kimesokitishwa na wale wote waliokuwa na nia mbaya au ovu
na kusababisha kwa siku ya tati mfurulizo Watu kukuosa huduma ya umeme
kuanzia tarehe 17 mwezi wa 5 hadi tarehe 20 mwaka huu.
"
Chama CCM kinaonya vikali kwa wale wote watendaji waliokuwa na nia
mbaya kwa wananchi,kwani wananchi Wamepata hasara kwa kitendo hicho cha
kukuza umeme kwa muda wa siku tati," amesema .
Sambamba
na hayo amesema Ili kuwa na Nishati ya kutosha Chama Cha Mapinduzi
kinaelekeza miradi yote ya usafirishaji, usambazaji unatekeleza kwa
haraka.
Pia amesema vijiji na vitongoji vote vilivyoachwa katika usambazaji vipate umeme na umeme uwe wa gharama za chini.
MAFUTA NA GESI ASILIA
Amempongeza
Rais wa Awamu ya Sita Samia Suluhu Hassan kwa juhudi zake katika
kuhakikisha Ujenzi wa bomba kubwa la Mafuta inafanyikia kutaka Hoima
nchini Uganda mpaka Tanga nchini Tanzanaia.
No comments:
Post a Comment