Na Jasmine Shamwepu, Dodoma
WAZIRI wa Mambo ya Ndani ya Nchi, George Simbachawene amesema Serikali itazichukulia hatua kali Jumuiya zote zilizopo chini ya Wizara yake ambazo zitakiuka sheria na taratibu katika kujiendesha.
Akizungumza leo Jijini Dodoma na Shirikisho la Wamiliki na Mameneja wa Shule na Vyuo binafsi nchini (TAMONGSCO), Waziri Simbachawene amesema wale ambao wamekuwa na utaratibu wa kuleta vurugu na kuzivuruga Jumuiya, Wizara yake itachukua hatua kali ambapo amedai ikiwezekana hata pingu zitatumika.
Aidha amesema Jumuiya hizo zilizoanzishwa na zinazofanya mambo mazuri katika nchi haiwezekani mtu mmoja akaleta ugumu hivyo Wizara itachukua hatua za kisheria na mwenye kuchukua hatua hizo ni yeye Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi.
Kwa upande wake,Mwenyekiti wa Shirikisho la Wamiliki na Mameneja wa Shule na Vyuo Binafsi nchini (TAMONGSCO), Alfred Luvanda amesema wanamshukuru Waziri kwa kusimamia zoezi la uchaguzi wa kuwapata viongozi wapya wa Shirikisho hilo halali ambapo amedai sasa watakuwa na uhuru wa kufanya Mambo yao huku Naibu Katibu Mkuu wa Shirikisho hilo,Youstor Ntungi akieleza Changamoto ya baadhi ya wenye shule kuchukuliwa kama wafanyabiashara kwa kutozwa kodi nyingi wakati wao wapo kwenye lengo la kutoa huduma ya kumsaidia mtoto yoyote wa Mtanzania.
No comments:
Post a Comment