Na Jasmine Shamwepu, Dodoma
Chama cha Wafanyakazi wa serikali na Afya Tanzania[TUGHE] kimeishauri na mifuko ya jamii kutoa elimu ya kutosha kwa wadau na wanachama wote wa mifuko ya hifadhi ya jamii kabla ya kufikia mwisho wa kipindi cha mpito na kabla ya kufikia kanuni mpya kujikita zaidi kutoa elimu ili kuondoa kuzusha migogoro inayoweza kujitokeza.
Hayo yamebainishwa jijini Dodoma na Mwenyekiti wa Chama cha Wafanyakazi wa serikali na Afya Tanzania[TUGHE] Taifa Archie Mntambo katika mkutano wa Baraza kuu maalum mwaka 2021 ambapo amesema hali hiyo itasaidia kuondoa taharuki na migogoro kama ilivyojitokeza mwaka 2018.
’’Tunaamini kuwa elimu zaidi ikitolewa kwa wadau wote wa mifuko ya hifadhi ya jamii nchini hasa wanachama waliokuwa kwenye mifuko hiyo ya hifadhi za jamii hakutakuwa na migogoro ya kupinga kanuni mpya zitakazotangazwa”amesema.
Aidha,Mwenyekiti huyo wa TUGHE Taifa amebainisha matarajio ya TUGHE kwa serikali ni kuhakikisha wastaafu wote wanapata stahiki bora na itazingatia mapendekezo yake pamoja na wadau na wanachama namna bora ya kufikisha taarifa katika bila kuleta mgogoro wowote.
‘’Ni matarajio yetu katika miaka mitatu iliyobaki hadi 2023 kuelekea kipindi cha mwisho cha mpito serikali itazingatia mapendekezo yake namna bora ya kufikisha taarifa kwa wadau wake bila kuleta taharuki’’amesema.
Sanjari na hayo, Mntambo ametumia fursa hiyo kumpongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Samia Suluhu Hassan kwa kusikiliza kilio cha muda mrefu cha wafanyakazi katika nyongeza ya mshahara na kupandishwa madaraja kwa mujibu wa sheria .
‘’Tunamshukuru Rais wa Tanzania Samia Suluhu Hassan kwa kupokea hoja za watumishi ambapo tayari ameshatoa maelekezo juu ya kupandishwa vyeo na madaraja‘’amesema.
Mkutano mkuu huo wa Baraza kuu Maalum, Chama cha Wafanyakazi wa serikali na Afya Tanzania[TUGHE] 2021 umekwenda sambamba na kaulimbiu isemayo ''Huduma bora Maslahi Zaidi.
No comments:
Post a Comment