HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

June 22, 2021

MAADHIMISHO KUPINGA MATUMIZI YA DAWA ZA KULEVYA

 

 

Mkurugenzi Mtendaji Tume ya Kitaifa ya Kuratibu  na Udhibiti wa Dawa za Kulevya, Luteni Kanali, Burhani Zuberi Nassor.

 

Mkurugenzi Mtendaji Tume ya Kitaifa ya Kuratibu  na Udhibiti wa Dawa za Kulevya akizungumza na waandishi wa habari.


Wazanzibari wasipokuwa wazalendo wa kupinga matumizi ya Dawa za Kulevya na  kuyadhibiti yasiingie nchini baada ya miaka 20 kila nyumba  itakuwa na mteja anaetumia Dawa za Kulevya na Taifa litateketea  

 Vijana wanaotegemewa ndio waathirika wakubwa wa matumizi ya dawa za kulevya hali hii isipoidhibitiwa na kushirikiana pamoja Taifa litateketea

Mkurugenzi Mtendaji wa Tume ya Kitaifa ya Kuratibu na  Udhibiti Dawa za Kulevya Luteni Kanali Burhani Zuberi Nassor ameyasema hayo wakati akizungumza na waandishi wa habari katika wiki ya kilele cha maadhimisho ya kupinga matumizi ya Dawa za Kulevya

Luteni Kanali Burhani amesema katika kukabiliana na janga hili  hatua madhubuti zinachukuliwa na Tume ili  kuhakikisha wanawadhibiti waingizaji, wauzaji na wasambazaji pamoja na watumiaji wa dawa za kulevya nchini

Tume ya Kitaifa ya Kuratibu na Udhibiti wa Dawa za Kulevya imejipanga vyema na wanahakikisha wale wote wanaojihusisha na madawa ya kulevya wanapelekwa kwenye vyombo vya sheria

Luteni Kanali Burhani amewahakikishia wananchi kuwa mikakati mipya imeandaliwa na sheria inafanyiwa marekebisho ili kuweza kuchunguza, kupeleleza, kukamaata na kupeleka mahakamani.

‘Tunahakikisha tunatoka hapa tulipo na kubadilisha Sheria pamoja na  Muundo  badala ya Tume iliyopo inabadilika na kuwa Mamlaka kamili ili kuweza kuzisimamia vyema sheria kwani Zanzibar bila ya dawa za kulevya inawezekana iwapo sote tutashirikiana’

Pia amesisitiza kuwa na dhamira thabiti ya kuchukia na kuondoa dawa za kulevya jambo ambalo litalipelekea Taifa hili kufika mbali kiuchumi hivyo ni wajibu wa kila mmoja kusimamia sheria kuanzia viongozi, wananchi, shehia, Halmashauri, vyombo vya ulizi na usalama, Wilaya na Mkoa kwa kutii sheria bila shuruti

Ameeleza kuwa wahalifu wanaishi ndani ya shehia zetu hivyo lazima kuwepo na mashirikiano na jamii ili kuwaibuwa wanaoliangamiza Taifa hili kwa kuondoa muhali na kutoa taarifa za uhalifu wa dawa ya kulevya.

‘Tukithubutu kushirikiana na kubadilisha mifumo ya maisha ambayo tunaishi ya usasa ni wazi sula la matumizi ya madawa ya kulevya hapa kwetu litakuwa ni historia, wazazi na walezi pia tuwe wadadisi wa watoto wetu na kufatilia mwenendo wao, mtoto anakuja na vespa au pikipiki mzazi huulizi anarudi usiku huulizi anavitoa wapi vitu vya thamani hizi ni dalili mbaya na  turudi kwenye malezi yaasil’ alisisitiza

Akitoa takwimu Mkurugenzi Uchunguzi na Udhibiti Ndugu Juma A. Zidikheri kupitia ripoti ya kitengo cha Polisi cha Kupambana na Dawa za Kulevya kwa kipindi cha miaka 9 iliyopita 2012-2020 jumla ya watuhumiwa 3,810 wakiwemo wanaume 3,577 na wanawake 233 wamekamatwa nchini wakijihusisha na Dawa za Kulevya

Aidha katika kipindi hicho jumla ya kilo 51.5 za heroini, kilo 2,946 za bangi, kilo 5.4 za Valium na kilo 19.71 za kokeni zilizokamatwa

Mkutano na waandishi wa habari umefanyika kwenye ukumbi wa mkutano Ofisi ya Makamu wa Kwanza wa Rais pia umehudhuriwa na wakurugenzi kutoka ofisi hio akiwemo Mkurugenzi Mipango, Sera na Utafiti Bi Daima M. Mkalimoto na Mkurugenzi Uendeshaji na Utumishi Ndugu Juma Ali Simai 

Mkutano wa Kilele cha Maadhimisho ya wiki ya kupinga Matumizi ya Dawa za Kulevya utafanyika siku ya Jumamosi tarehe 26/06/2021 katika ukumbi wa Sheikh Idriss Abdulwakil Kikwajuni na mgeni rasmi ni Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe Dkt Hussein Ali Mwinyi

Ujumbe wa Mwaka huu ni ‘Sema Ukweli juu ya athari za Dawa za Kulevya Okoa Maisha ’

No comments:

Post a Comment

Pages