HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

June 22, 2021

VIJANA MKOANI KAGERA WATAJWA KUPIGA TEKE MASUALA YA KILIMO WENGI KUKIMBILIA BODA BODA

 


Na Lydia Lugakila, Bukoba

Kauli hiyo imetolewa na Mkuu wa Mkoa wa Kagera Meja Jenerali Charles Mbuge katika hafla ya kuwaapisha wakuu wa wilaya wapya wa mkoa huo iliyofanyika katika ukumbi wa ofisi za mkoa huo.

Meja Jenerali Charles Mbuge amesema  vijana wengi mkoani humo hawajishughulishi na shughuli za uzalishaji mali ambapo wamepiga teke suala la kilimo na kukimbilia uendeshaji wa pikipiki maarufu Boda Boda huku utayari wa kupokea fursa zinazotoka katika wilaya zao likiachwa nyuma jambo alilolitaja kama changamoto mkoani humo.

Meja Jenerali Mbuge amesema mkoa wa Kagera una fursa nyingi ikiwa ni pamoja na shughuli za uzalishaji mali  kama kilimo, uvuvi

" Vijana mnatakiwa kukubali kupokea fulsa zinazoto katika wilaya zenu wengi mmekimbilia Boda Boda jaribu kutambua fulsa undeni vikundi mkanufaike" alisema Meja Jenerali Mbuge.

Mkuu huyo wa mkoa ametumia nafasi hiyo kuwahimiza wakuu wa wilaya wapya walioteuliwa kuhakikisha wanasimamia miradi kwa weledi, kutenga muda kusikiliza kero za wananchi waliopo katika maeneo yao, kusimamia masuala ya ulipaji kodi bila upendeleo pamoja na kusimamia miradi mbali mbali ya maendeleo na kuhakikisha inakamilika kwa wakati.

Aidha ameongeza kuwa  mkoa wa Kagera upo katika nafasi ya  asilimia 88 katika ukusanyaji wa kodi na asilimia 95 ni kodi za ndani huku akipongeza upande wa forodha kufanya vizuri na kuwa katika kiwango Cha asilimia 103.

Kwa upande wake mkuu wa wilaya ya Bukoba Moses Machali amewaomba wananchi Mkoani Kagera kushirikiana na viongozi katika shughuli za maendeleo ili kuinua mkoa huo na taifa kwa ujumla.

Hata hivyo wakuu wa wilaya za mkoa huo walioapishwa ni pamoja  na mkuu wa wilaya ya Misenyi Wilson Sakulo Julieth Binyula mkuu wa wilaya ya Karagwe na Kemilembe Lwota mkuu wa wilaya ya Biharamulo.

No comments:

Post a Comment

Pages