Makamu wa Kwanza wa Serikali ya Umoja wa Kitaifa Zanzibar (SUK), Masoud
Othman Masoud akisalimia wna kuzungumza na wajumbe wa Kamati Kuu ya
Chama cha ACT-Wazalendo alipowasili kwenye Hoteli ya Lamada kushiriki
Kikao cha Kamati Kuu ya Kawaida kinachofanyaka hotelini hapa leo.
Makamu wa Kwanza wa Serikali ya Umoja wa Kitaifa Zanzibar (SUK), Masoud
Othman Masoud akisalimiana na viongozi wa Chama cha ACT-Wazalendo
alipowasili kwenye Hoteli ya Lamada kushiriki Kikao cha Kamati Kuu ya
Kawaida kinachofanyaka hotelini hapa leo.
Na Mwandishi Wetu
MAKAMU
wa Kwanza Rais wa Serikali ya Umoja wa Kitaifa Zanzibar (SUK), Masoud
Othman Masoud ameahidi kufanya kazi kwa kujituma ili kufanikisha malengo
ya Chama cha ACT-Wazalendo na nchi.
Makamu
huyo alitoa kauli hiyo leo Juni 19/2021 wakati akizungumza kwa mara ya
kwanza kama mjumbe wa Kamati Kuu ya Chama cha ACT-Wazalendo kwenye kikao
cha kamati kuu cha kawaida kinachofanyika katika Ukumbi wa Lamada Ilala
jijini Dar es Salaam.
Pamoja
na Masoud pia Kaimu Mwenyekiti wa ACT-Wazalendo Dorothy Semu
aliwatambulisha wajumbe wapya wa Kamati Kuu ambao ni Mwenyekiti wa
Wabunge wa Bunge la Wawakilishi Hassan Hamad Omar na Khalifa Mohammed
Omar Mwenyekiti wa Wabunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano Tanzania.
Amesema
nafasi aliyopewa na chama hicho ya kuwa Makamu wa Kwanza wa Rais wa
Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar (SMZ), imemuheshimisha hivyo
atahakikisha anaitendea haki ili kuwe na matokeo chanya.
"Tupo
wengi ndani ya chama na wengine wazito kuliko mimi lakini mliona mimi
ndiye nichukue nafasi baada ya kifo cha Mwalimu na Kiongozi wetu Hayati
Maalim Seif Sharif Hamad niseme wazi nitajitahidi kwa kila njia
kuhakikisha siwaangushi.
Nakumbuma
alikuja Katibu na Makamu Mwenyekiti kuniambia natakiwa kuwa Makamu wa
Kwanza wa Rais niliwajibu hivi mnajua mimi ni fundi Seremala hivyo fundi
Uwashi sitoweza wakanijibu kuwa naweza hivyo kwa maslahi ya chama
nilikubali na kazi zinaendelea," amesisitiza.
Masoud
amesema kukubali nafasi hiyo ilikuwa mtihani mzito ila anaamini
waliomuana waliona uwezo wake hivyo akasisitiza ushirikiano ndani ya
chama na serikali ili kuchochea maendeleo na mshikamano.
Aidha, Masoud amewataka wana ACT kutosista kumrekebisha iwapo wataona anapotoka kwa kuwa hakuna mtu mkamilifu.
Makamu
wa Rais huyo amesema anashukuru chama chake kumpitisha katika nafasi
hiyo ya ujumbe wa kamati kuu kwani atakuwa amekamilisha utekelezaji wa
majukumu yake kwa sasa.
Masoud amesisitiza mshikamano kwa viongozi na wanachama ili kuchochea maendeleo.
No comments:
Post a Comment