HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

June 19, 2021

SERIKALI YAAHIDI MABORESHO TAASISI ZA UTOAJI HAKI

 Na Jasmine Shamwepu, Dodoma

 
SERIKALI imesema imeazimia kuendelea kuimarisha taasisi zote za utoaji haki hasa Mahakama, pamoja na kutatua changamoto  zinazoikabili sekta hiyo, hasa uhaba wa watumishi, huku akiwataka Wanasheria wote wa Umma nchini kuhakikisha wanafanya mashauriano na Ofisi ya Wakili Mkuu wa Serikali kabla ya kuanza kesi, ili kushinda.

 
Kauli hiyo imetolewa leo jijini Dodoma na Waziri wa Katiba na Sheria, Profesa Paramagamba Kabudi, wakati akifungua mkutano wa kwanza wa Watumishi wa Ofisi ya Wakili Mkuu wa Serikali na kusema Serikali itahakikisha inazifanyia kazi changamoto zote.

Aidha amesema katika kufanya mashauri yote kupitia ofisi ya wakili wa Serikali itasaidia wao kujipanga kisheroia katika mashauri yao.

Hata hivyo ametaka  kuona umuhimuwa matumizi ya lugha ya Kiswahili  katika mahakama kwakuweka istilahi na misamiati ya kisheria katika suala zima la uendeshaji kesi.

 

Kwa upande wake Wakili Mkuu wa Serikali,Gabriel Malata ameiomba Serikali kupitia Wizara ya Katiba na Sheria kuwapa mafunzo ili kuwajengea uwezo katika uendeshaji wa madai ya Gesi na Madini katika kuelekea uchumi wa Viwanda kutokana na wanasheria wengi kutokuwa na uelewa wa masuala hayo.


Sambamba na hilo ameeleza changamoto mbalimbali ikiwemo uhaba wa watumishi na Vitendea kazi ikiwemo watumishi walipo ni 143 huku mahitaji ni 312.

No comments:

Post a Comment

Pages