HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

June 04, 2021

MAVUNDE AANZA KUBORESHA MIUNDOMBINU VIWANJA VYA MICHEZO

 


Mbunge wa Jimbo la Dodoma Mjini, Mhe. Anthony Mavunde akikabidhi vifaa vya michezo vyenue thamani ya Tsh. Milioni 3 kwa Wanafunzi wanaounda timu ya Jiji la Dodoma.



Na Mwandishi Wetu, Dodoma

MBUNGE wa Jimbo la Dodoma Mjini, Mhe. Anthony Mavunde katika azma yake ya kukuza michezo ngazi ya chini, ameanza kuboresha miundombinu ya viwanja vya michezo katika shule za. Msingi na Sekondari za Jiji la Dodoma ili kuwaandaa wanafunzi wenye vipaji.

Mhe. Mavunde amekabidhi vifaa vya michezo vyenye thamani ya Sh 3,000,000 kwa wanafunzi wanaounda Timu ya Jiji la Dodoma wanaoshiriki  mashindano ya UMISETA ngazi ya Mkoa.

Akikabidhi vifaa hivyo, Mavunde amewahakikishia wanafunzi hao kuwawekea miundombinu bora katika viwanja vya shule zao wanavyotumia kwa ajili ya michezo mbalimbali.

"Nimefurahi kujumuika hapa nanyi leo ikiwa ni hafla fupi ya kuwakabidhi vifaa vya michezo na kuwatakia kila la kheri katika mashindano yenu ya UMISETA ngazi ya mkoa.

"Ningependa kuona Jiji la Dodoma linakuwa mbele katika kila jambo ikiwemo michezo, hivyo ni imani yangu kwamba mtafanya vizuri katika mashindano haya ya mkoa.

"Ninaendelea kuboresha miundombinu ya viwanja katika shule zenu kwa kuweka magoli ya chuma na kukarabati baadhi ya viwanja. Katika awamu ya kwanza naanza na shule 20 za msingi na sekondari na baadaye tutamalizia katika viwanja vilivyobaki," amesema Mavunde.

Pamoja na mambo mengine, Mavunde ametumia fursa hiyo kuwatakia heri na mafanikio Timu ya UMITASHUMTA ya Mkoa wa Dodoma ambayo inajiandaa na safari ya kuelekea Mtwara kushiriki mashindano ya UTAMITASHUMTA ngazi ya Taifa na kuwaahidi kiasi cha Sh 2,000,000 endapo watashinda michezo mitano.

Akizungumza kwa niaba ya Ofisa Elimu wa Sekondari Jiji la Dodoma, Mwalimu Upendo Rweyemamu amemshukuru Mbunge Mavunde kwa kufadhili vifaa vya michezo kwa timu za wanafunzi za Jiji la Dodoma kila mwaka na kumuahidi ushindi katika michezo yote ili kulinda heshima ya jiji hilo.

No comments:

Post a Comment

Pages