Kaimu Mkaguzi Mkuu wa Ndani Benki ya NMB, Benedicto Baragomwa, akizungumza wakati wa uzinduzi wa 'NMB Healthcare Club,' uliofanyika Dar es Salaam.
Mganga Mkuu wa Serikali, Dk. Aifelo Sichwale, akitoa hotuba yake wakati wa
uzinduzi wa 'NMB Healthcare Club,' uliofanyika Dar es
Salaam.
Mganga Mkuu wa Serikali Dk. Aifelo Sichwale (kushoto), akipata maelezo kutoka kwa, Elizabeth Lema ambaye ni Mkurugenzi wa Kampuni ya Cornwell Tanzania inayojihusisha na utengenezaji wa dawa za asili na virutubisho, wakati wa uzinduzi wa 'NMB Healthcare Club,' uliofanyika Dar es Salaam jana. Wa pili kutoka kushoto ni Kaimu Mkaguzi Mkuu wa Ndani Benki ya NMB, Benedicto Baragomwa.
Mganga Mkuu wa Serikali Dk. Aifelo Sichwale (wa pili kushoto), akipata maelezo kutoka kwa mwakilishi wa Chama cha Wanasayasi wa Maabara za Afya Tanzania (MELSAT), Godfrey Hongoli (kulia), wakati wa uzinduzi wa 'NMB Healthcare Club,' uliofanyika Dar es Salaam. Kushoto ni Kaimu Mkaguzi Mkuu wa Ndani Benki ya NMB, Benedicto Baragomwa.
NA MWANDISHI WETU
BENKI
ya NMB, imekuwa ya kwanza nchini kuzindua 'NMB Healthcare
Club,' mtandao unaowapa wadau wa Sekta ya Afya mikopo ya vifaa kazi,
mitaji na uwekezaji, huduma inayokuja huku benki hiyo ikiwa imetumia
zaidi ya Sh. Bilioni 32 kutoa mikopo kwa Sekta Binafsi ya Afya, kati ya
Sh. Bilioni 112.5 ilizopanga kutumia hadi mwaka 2025.
NMB
Healthcare Club imezinduliwa sambamba na Kongamano la Afya 'Tanzania
Health Summit 2021,' uzinduzi uliowakutanisha wadau wa Sekta ya Afya
zaidi ya 150, wakiwemo madaktari, wamafasia, wamiliki wa hospitali,
zahanati, vituo na vyuo mbalimbali vya afya na viongozi wa vyama
washirika.
Uzinduzi huo
umefanyika mwishoni mwa wiki jijini Dar es Salaam, ambako Mganga Mkuu wa
Serikali Dk. Aifelo Sichwale, aliyemwakilisha Katibu Mkuu wa Wizara ya
Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, aliipongeza NMB kwa
kuwaunganisha na kuwapa uwezeshaji wadau muhimu wa Sekta ya Afya nchini.
Akizungumza
wakati wa uzinduzi huo, Dk. Sichwale alibainisha kuwa, wajibu wa kutoa
huduma kwa wananchi, zikiwamo za afya ni wa Serikali, lakini fursa na
uwezo havitoshelezi, hivyo kufungua milango kwa Sekta Binafsi ya Afya na
kwamba wataendelea kushirikiana na wadau wote wanaohudumu katika sekta
hiyo.
"Uzinduzi huu
unaofanyika leo una baraka zote za Serikali na tunawaunga mkono NMB kwa
juhudi zenu za kuwaunganisha madaktari na wadau wengine muhimu wa Sekta
ya Afya hapa nchini, katika kusapoti malengo ya Serikali ya Rais Samia
Suluhu Hassan ya kuboresha mazingira ya sekta hii.
"Malengo
ya Serikali ni kuboresha mazingira ya wafanyabiashara kushiriki kukuza
Uchumi wa Taifa kupitia kodi wanazolipa, kutoa ajira na kuongeza mitaji.
Tunaamini kupitia NMB Healthcare Club, wanachama watapata mafunzo
kuhusu maarifa ya kibiashara pamoja na elimu kifedha," alisema Dk.
Sichwale.
Aliipongeza NMB
sio tu kwa kuwaunganisha wadau hao muhimu, bali utayari wao wa kutoa
bure elimu ambayo mahali pengine wangeipata kwa gharama kubwa, hasa juu
ya uwekaji akiba, uwekezaji, umuhimu wa kupitisha fedha zao kwenye
akaunti ya benki, pamoja na huduma zinginezo
Naye
Kaimu Afisa Mkaguzi Mkuu wa Ndani wa Benki ya NMB, Benedicto Baragomwa,
aliwapongeza wadau wa Sekta ya Afya kwa mapambano katika kipindi cha
janga la COVID-19, na kwamba wao kama benki waliwaunga mkono wateja wao
kwa kuwapa ahueni za kifedha na kubadili mfumo wa urejeshaji wa mikopo
yao.
"Ukaribu wetu kwa
wateja ulilenga kuwawezesha kuhimili changamoto zilizotokana na janga la
Corona. Kwa sababu sisi NMB tumekuwa mstari wa mbele katika kusaidia
sekta hii ya afya, ambako tunatoa misaada ya vifaa tiba, vikiwamo
vinavyolenga kuhudumia eneo lenye changamoto nyingi, la afya ya uzazi.
"NMB
tumeingia kwa nguvu moja kuhakikisha huduma bora za afya zinapatikana
kwa wote, ambapo kupitia huduma ya Asset Financing - inayotoa mikopo
nafuu mahsusi kwa Sekta Binafsi ya Afya, tumetumia zaidi ya Sh. Bilioni
32 Hadi Machi mwaka huu, kati ya Sh. Bilioni 112.5 tulizopanga kutumia
hadi mwaka 2025.
Kwa
upande wake, Rais wa Tanzania Health Summit, ambaye pia ni Mkuu wa Idara
ya Phisiolojia Chuo Kikuu Cha Afya na Sayansi Shirikishi Muhimbili
(MUHAS), Dk. Omary Chillo, aliiomba Serikali kuongeza nafasi za wadau wa
Sekta Binafsi ya Afya kushiriki vikao vya mipango kazi wizarani.
Naye
Rais wa Chama cha Madaktari Tanzania (MAT), Shedrack Mwaibambe,
aliitaja NMB kama benki ambayo haijawahi kuacha kujaribu katika kila
eneo kuhakikisha inaikwamua Sekta ya Afya Tanzania, na kwamba NMB
Healthcare Club ni uthubutu mwingine unaowapa nguvu za ziada wawekezaji
na wadau muhimu waliopo katika sekta hiyo.
No comments:
Post a Comment