Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Mwigulu Nchemba akiongoza Kikao kazi cha Wadau wa Sekta ya Fedha nchini kuhusu Sekta binafsi zikiwemo Benki kushiriki katika kutekeleza miradi ya maendeleo, katika ukumbi wa Wizara ya Fedha na Mipango, jijini Dodoma.
SAIDINA MSANGI NA PETER HAULE, WFM
SERIKALI
imefungua wigo kwa sekta binafsi kushiriki katika utekelezaji wa miradi
ya kimkakati ili kufanikisha utekelezaji wa malengo ya Mpango wa Tatu
wa Maendeleo wa Taifa wa Miaka Mitano 2021/22-2025/26 unaotarajiwa
kuzinduliwa hivi karibuni.
Hayo
yameelezwa jijini Dodoma na Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dk.
Mwigulu Lameck Nchemba (Mb), alipokutana na wadau na taasisi za fedha
nchini katika kikao kilichoangazia ugharamiaji wa miradi ya maendeleo
kwa njia mbadala.
Akizungumza
katika kikao hicho Dk. Nchemba alisema kuwa tathmini iliyofanyika ya
utekelezaji wa Mpango wa Pili wa Maendelo wa Taifa ilibainisha ushiriki
mdogo wa sekta binafsi katika utekelezaji wa mpango huo hivyo Serikali
imeona ijadiliane nao kuona namna bora ya kuwezesha ushiriki wa sekta
binafsi katika Mpango wa Tatu wa Taifa wa Maendeleo.
“Tuliona
tujadiliane tunapokwenda kuanza mwaka mpya wa fedha na tukijua tuna
miradi ya kitaifa inayoendelea tuanze kwa pamoja kwa kuangalia njia
mbadala tunazoweza kutumia kufanikisha utekelezaji wa miradi ya
maendeleo,”alisema.
Alisema
kuwa kuna umuhimu wa kuwa na njia mbadala za kuwezesha utekelezaji wa
miradi mikubwa ya maendeleo ili isiathiri utekelezaji wa shughuli za
utoaji wa huduma za kijamii, ikiwemo elimu, maji na afya.
Alifafanua
kuwa kwa upande wa miradi inayoweza kutekelezwa kwa njia mbadala
Serikali itaboresha mazingira ya kuwezesha utekelezaji wa miradi hiyo
kupitia sekta binafsi kwa kuhakikisha inafanyia kazi baadhi ya hoja
zilizoibuliwa katika kikao hicho ikiwemo masuala ya kiutawala.
Akizungumza
wakati akimkaribisha Waziri wa Fedha na Mipango, Katibu Mkuu wa Wizara
hiyo na Emmanuel Tutuba alisema, kuwa Serikali imeshirikisha sekta
binafsi ili kupata fedha nyingi zaidi kwa ajili kutekeleza miradi ya
maendeleo kwa wakati.
Alisema
kuwa Serikali inatarajia mchango mkubwa kutoka sekta binafsi katika
utekelezaji wa Mpango wa Maendelo wa Taifa wa Tatu na kuwa itaendelea
kupokea maoni na mawazo kutoka sekta binafsi ili kuwezesha utekelezaji
wa miradi mingi zaidi.
“Nitoe
wito kwenu kuwasilisha wizarani maeneo mnayohitaji maboresho ya kisera
na kikodi ili yaweze kufanyiwa kazi kwa mujibu wa sheria ili kufanikisha
ushiriki wenu kikamilifu katika utekelezaji wa miradi ya maendeleo,”
alisema Tutuba.
Aidha
Tutuba ametoa wito kwa wadau hao kutoa ushirikiano kwa Serikali na
kukaribisha wawekezaji kutoka nje ili nao waweze kuona maeneo wanayoweza
kushiriki katika utekelezaji wa miradi mikubwa na midogo iliyo katika
mpango huo.
Naye Kamishna
wa Idara ya Uendelezaji wa Sekta ya Fedha Dk. Charles Mwamwaja alisema,
kuwa dirisha hilo litatoa fursa kwa Serikali kupata fedha kutoka vyanzo
vya ndani kutatua changamoto ya upatikanaji wa fedha za miradi na
kuharakisha utekelezaji wa miradi ya maendeleo itakayojumiisha maeneo
mengi zaidi.
“Mpango huo
utasaidia katika kuongeza ufanisi wa utekelezaji wa miradi ya maendeleo
huku ikitoa fursa kwa Serikali kujielekeza katika maeneo mengine ya
vipaumbele ambayo sekta inafsi haiwezi kufika,”alisema Dk. Mwamwaja.
Alifafanua
kuwa Mpango wa Tatu wa Maendeleo wa Taifa umebainisha kiwango cha fedha
kitakachohitajika katika utekelezaji wa miradi ambapo Serikali
inatarajia kukusanya kiasi cha Sh. trilioni 74.3 katika vyanzo vyake na
kiasi cha Sh.40.6 kinatarajiwa kupatikana kutoka vyanzo mbadala ikiwemo
Sekta Binafsi.
Kwa upande
wa sekta binafsi, imepongeza hatua ya Serikali kufungua rasmi dirisha
la ushiriki wa sekta binafsi katika utekelezaji wa miradi ya maendeleo
na kubainisha kuwa wako tayari kushiriki kikamilifu katika utekelezaji
wa mpango huo.
Wamepongeza
pia uamuzi wa Serikali wa kuboresha mazingira ya ufanyaji biashara na
uwekezaji hatua inayiwapa Imani ya kuwekeza mitaji na fedha zao katika
ujenzi wa miradi hiyo yenye lengo la kuboresha maisha ya watu na kukuza
uchumi wa nchi.
No comments:
Post a Comment