HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

June 15, 2021

TANZANIA YAENDELEA KUNG'ARA KWENYE UTALII BARA LA AFRIKA

 

Waziri wa Maliasili na Utalii, Dkt. Damas Ndumbaro akizungumza katika mkutano wa Kimataifa wa Utalii wa kanda ya Afrika ulioandaliwa na Shirika la  Umoja wa Mataifa la Utalii (UNWTO) unaofanyika kwa muda wa siku tatu katika Jiji la Windhoek nchini Namibia.


Waziri wa Maliasili na Utalii, Dkt. Damas Ndumbaro akifanya  kikao cha ana kwa ana  na mbobezi  wa kimataifa wa kutangza vivutio vya Utalii kutoka Shirika la Umoja wa Kimataifa  la Utalii (UNWTO) Bi. Olgo Nowak mara baada ya kufanya  wasilisho lake ambapo Tanzania imetajwa kung'ara 10 bora miaka mitatu mfululizo kuanzia 2017 hadi mwaka 2020. (Katikati)  ni Kamishna Msaidizi Maendeleo ya Biashara kutoka Shirika la Hifadhi za Taifa, Bi. Beatrice Kessy
 
Kamishna Msaidizi Maendeleo ya Biashara, Bi. Beatrice Kessy  kutoka Hifadhi za Taifa (TANAPA)  akizungumza wakati wa mkutano wa Kimataifa wa Utalii wa Kanda ya Afrika ulioandaliwa na Shirika la  Umoja wa Mataifa la Utalii (UNWTO).

 


NA MWANNDISHI WETU, WINDHOEK, NAMIBIA

TANZANIA imeendelea kung'ara ndani ya Bara la Afrika kwa kutangaza vyema vivutio vyake vya Utalii ambapo imeweza kuwa miongoni mwa nchi10 bora kwa mwaka wa tatu mfululizo, kuanzia 2017 hadi  2020.

Ripoti hiyo imetolewa mapema jana 14 Juni kwenye mkutano wa Kimataifa wa Utalii wa Kanda ya Afrika ulioandaliwa na Shirika la Kimataifa la Utalii  Duniani  (UNWTO), kupitia kwa Mtaalamu wa utangazaji wa Utalii, Bi. Olga Nowak aliitangaza Tanzania kushika nafasi ya Saba  ambayo inakuwa ni mara ya tatu.

Katika mkutano huo, Waziri wa Maliasili na Utalii, Dkt. Damas Ndumbaro akiwa ameambatana na Watalaamu wake kutoka Wizara ya Maliasili na Utalii ambapo Waziri Dkt. Ndumbaro amesema Tanzania imejaliwa kuwa na vivutio vingi na vya kipekee ambavyo havipatikani mahali popote duniani isipokuwa Tanzania.

Katika kumi bora hiyo,   Afrika ya Kusini imetajwa kushika nafasi ya kwanza ikifutiwa na nchi ya  Misri  katika utangazaji vyema  ya vivutio vyake vya  utalii.

Aidha katika ripoti hiyo, Tanzania imetajwa  kuendelea kuongoza na kufanya vizuri katika sekta ya utalii licha ya uwepo wa changamoto wa ugonjwa wa UVIKO19  ambao umeikumba karibu Mataifa mbalimbali duniani kote.

Tanzania imekuwa na vivutio mbalimbali vinavyotamba Duniani ikiwemo mlima mrefu barani Afrika, Mlima Kilimanjaro, Hifadhi zenye vivutio vikubwa vya Wanyama kama Hifadhi ya Serengeti, Hifadhi ya Nyerere, Hifadhi ya Ruaha, Tarangile,l pamoja na Mamlaka ya Hifadhi ya Eneo la Ngorongoro.

Katika hatua nyingine  Tanzania kushiriki katika mkutano huo wa siku tatu,  kupitia Waziri wa Maliasili na Utalii, Dkt. Ndumbaro na wataalamu, imepata fursa ya kushirikiana na Jumuiya ya Kimataifa hususani viongozi wa Serikali na wadau wa utalii kutoka nchi wanachama wa UNWTO katika kukabiliana na athari za COVID-19 na kuandaa mikakati madhubuti ya kurejesha sekta ya utalii katika hali ya awali kwa kufanya vikao vya ana kwa ana na viongozi wanaoshiriki mkutano huo.

Aidha,Tanzania imepata  fursa ya kutoa maoni yake kwa lengo la kuimarisha utangazaji wa vivutio vya utalii vilivyopo Bara la Afrika ikizingatiwa kuwa Tanzania ni miongoni mwa nchi zenye vivutio vingi na vya kipekee katika Bara la Afrika ambapo Waziri Dkt. Ndumbaro amemkaribisha Mtaalamu wa masuala ya utangazaji kuja Tanzania kutoa ujuzi huo.

Kwa upande wake, Kamishna Msaidizi Maendeleo ya Biashara, Bi. Beatrice Kessy  kutoka Hifadhi za Taifa (TANAPA)  ambaye yupo kwenye mkutano huo, amesema Tanzania ni miongoni mwa nchi zenye vivutio vingi na vya kipekee Barabi Afrika ambapo ameomba ushirikiano wa makampuni makubwa ya Kimataifa kuisaidia Tanzania  kutangaza vivutio vya utalii vilivyoko Tanzania ili viweze kujulikana na watu wengi duniani.

Ameongeza kuwa, ili kuongeza idadi ya watalii wataokatembelea Tanzania, Makampuni makubwa yanapaswa kuchangamkia fursa ya  kutembelea Tanzania ilikuweza kutangaza vivutio hivyo.

No comments:

Post a Comment

Pages