HABARI MSETO (HEADER)


July 10, 2021

BARAZA LA TAIFA LA MASHIRIKA YASIYO YA KISERIKALI LAZINDULIWA

 


Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto Dkt.Dorothy Gwajima akizungumza na viongozi wa Baraza la Mashirika Yasiyo ya Kiserikali (NACONGO) wakati wa uzinduzi wa Baraza hilo jijini Dodoma.


Baadhi ya wajumbe wa Baraza jipya la Mashirika Yasiyo ya Kiserikali (NACONGO) wakifuatilia hotuba ya Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Dorothy Gwajima alipokuwa akizundua Baraza hilo jijini Dodoma.

   

Na Jasmine Shamwepu, Dodoma

Waziri wa Afya maendeleo ya jamii,jinsia wazee na watoto Dkt Dorothy Gwajima amewataka viongozi na wajumbe wa Baraza la taifa la mashirika yasiyokuwa ta kiserikali (NaCoNGO) kufanya kazi kwa weledi, uadilifu na uzalendo wa hali ya juu ili kuleta tija katika taifa.


Hayo aliyasema Leo Jijini Dodoma wakati akipokea taarifa na kuzindua baraza la taifa la mashirika yasiyokuwa ya kiserikali NaCoNGO).


Amewataka kwenda kufanya kazi kwa kuzingatia Sheria na miongozo iliyopo ili kukidhi matarajio ya waliowachagua na jamii ya watanzania kwa ujumla.


"Napenda kuwasilisha nimepokea kwa mikono miwili taarifa ya kamati ya mpito kwani nimeisikiliza mapendekezo ya kamati ambayo wengine utekelezaji wake unahitaji kujitoa kwenu kwa Hali na Mali na mengine ni ya kwetu upande wa wizara" amesema Dkt Gwajima


Na kuongeza kusema kuwa "ikumbukwe kwamba Baraza la taifa la mashirika yasiyokuwa ya kiserikali ni chombo cha uwakilishi na kiungo muhimu kati ya mashirika na serikali hivyo kutofanyanyika kwa uchaguzi na kutokuwepo kwa Baraza kihali kulisababisha vyombo vya usimamizi wa mashirika ya kiserikali kushindwa kuteleza majukumu yake kwa mujibu wa Sheria.


Amesema nikiwa kama msimamizi wa Sheria na kanuni za mashirika yasiyo ya kiserikali nisingeweza kuvumilia vitendo vya ukiukwaji wa Sheria na kanuni hizo.


Hata hivyo amesema mashirika yasiyo ya kiserikali yamekuwa yakitekekeza miradi na afua katika maeneo mbalimbali ya kiutekelezaji ikiwa ni pamoja na sekta ya Afya,kilimo,elimu, maji,mazingira,utawala bora, nishati,uhifadhi wa jamii,uwezeshaji wa jamii na sekta nyingine.


Kwa Upande wake Mwenyekiti wa kamati ya Mpito ya uratibu na usimamizi wa uchaguzi wa NaCoNGO Flaviana Charles amesema wa
naishukuru serikali ya awamu ya sita Samia Suluhu Hassan na waziri wake kwa kuhakikisha  uchaguzi wa NaCoNGO inafanyika.


Alisema mchakato wa uchaguzi uliofanyika kwa kufuata kanuni Sheria na demokrasia licha ya ufinyu wa muda uliokuwepo lakini tumefanikisha Jambo hili.


"Kama kamati ya Mpito tunaenda kutoa mapendekeza Baraza lipange ratiba ya uchaguzi mapema kabla ya miaka 3 ili wadau wote waweze kujua ratiba sahihi ya uchaguzi ujao," amesema.



Naye Mwenyekiti mpya wa NaCoNGO Lilian Badi amesema mchakato wa uchaguzi haukuwa rahisi kwani ushindani ulikuwa mkubwa kutokana na muamko wa NGO,s katika ngazi zote za  wilaya Mkoa hadi Taifa.


" Sasa kazi iendelee kwani NaCoNGO hii ni kisayansi,uweledi,utendaji na uwajibikaji mengi tumeyaona  na sasa tunakwenda kuyafanyia kazi kwa kuimarisha mahusiano mazuri kati ya NGO,s na serikali," amesema.


No comments:

Post a Comment

Pages