Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Tanzania Mhe. Tulia Ackson akipata maelezo ya namna uchambuzi wa hali ya hewa unavyofanyika kwa njia ya modeli za kimahesabu kutoka kwa Mkurugenzi Mkuu wa TMA, Dkt. Agnes Kijazi wakati alipotembelea ofisi za TMA, Kituo Kikuu cha Utabiri, Ubungo Plaza, Dar es Salaam, Tarehe 09/07/2021.
Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Tanzania Mhe. Tulia Ackson akijionea hindi utabiri wa hali ua hewa kila siku unavyorekodiwa katika studio za TMA kwa ajili ya kuruka katika vyombo mbalimbali vya habari nchini wakati alipotembelea ofisi za TMA, Kituo Kikuu cha Utabiri, Ubungo Plaza, Dar es Salaam, Tarehe 09/07/2021.
Na Mwandishi Wetu
NAIBU Spika wa Bunge, Dk. Tulia Ackson, ametoa wito kwa vyombo vya habari kutenga muda wa kutosha wa kurusha taarifa za hali ya hewa mara kwa mara ili kusaidia wananchi kuzipata kwa wakati na kuzitumia kwa ufanisi.
Aidha, alieleza kuwa kutokana na muda wa habari ya hali ya hewa kuwa mfupi, taarifa zinatolewa kwa ujumla na kwa ufupi, kitu ambacho kinaweza kuathiri matumizi yake.
“Nitoe wito kwa vyombo vya habari kuangalia namna ambavyo watakuwa wanazitumia taarifa kutoka Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) na kuzitoa mara kwa mara ili kutusaidia sisi wananchi kujiandaa na kufanya maamuzi sahihi katika mipango yetu, tuangalie kama vyombo vingine vya habari vya mataifa ya nje, ukifungua kila wakati unaangalia hali ya hewa,” amesema Dk. Tulia wakati alipotembelea Makao Makuu ya Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA).
Aliendelea kusema kuwa, alichojifunza katika ziara yake fupi katika ofisi za Makao Makuu ya Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania, ni kuwa taarifa zipo, lakini kwa ajili ya muda mfupi basi Mamlaka inalazimika kuziweka katika huo muda mfupi.
Alitoa wito kwa wananchi kuitembelea mamlaka hiyo ili kujifunza masuala mbalimbali ikiwemo namna taarifa za hali ya hewa zinavyochakatwa kitaalamu hadi kumfikia mtumiaji.
No comments:
Post a Comment