Baadhi ya wanafunzi wakiwa katika banda la Chuo Kikuu cha Iringa (UOI).
Hussein Ndubikile, Dar es Salaam
Chuo
Kikuu cha Iringa (UOI) kimewakaribisha wanafunzi waliomaliza kidato cha
sita kujiunga na mwaka wa masomo wa 2021/22 kwani watafaidika na kozi
mbalimbali ikiwemo ya Shahada ya Masoko na Ujasiriamali itakayowasaidia
kukabiliana na tatizo la ajira kwa kuanzisha kampuni zao baada ya
kuhitimu masomo yao chuoni hapo.
Hayo yamesemwa
na Mhadhiri wa Chuo hicho Angel Ezekiel katika Maonesho ya 16 ya Elimu
ya Juu, Sayansi na Teknolojia yaliyoandaliwa na Tume ya Vyuo Vikuu
Nchini (TCU) yanayondelea kwenye Viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es
Salaam.
Amesema katika kukabiliana na tatizo
hilo wamejipanga kufundisha kozi kwa nadharia na vitendo ili kutengeneza
kundi kubwa la wahitimu wanaoweza kulimudu tatizo la ajira hapa nchini
kwani wataweza kuanzisha kampuni zao wenyewe.
"
Tunachanganya nadharia na vitendo kuendana na soko la ajira wanafunzi
watakaojiunga nasi watamaliza masomo yao wakiwa wanaweza kujiajiri
Barani Afrika ndio chuo kipekee kinachofundisha kwa vitendo masuala ya
biashara na ujasiriamali" amesema Angel.
Amebainisha
kuwa kupitia shahada hiyo wanafunzi wa mwaka wa kwanza wa masomo
watapata fursa ya kufundishwa jinsi ya kuanzisha biashara chini ya
usimamizi wa walimu waliobobea hivyo mara watakapohitimu wataendelea
nazo.
Ameongeza kuwa wanafunzi watakaosoma
taaluma ya Uhandishi wa Habari watafundishwa katika mazingira ya
nadharia na vitendo katika matukio yanayofanyika uoi kwani chuoni hapo
kuna radio ya Hope Fm, Gazeti la chuo pamoja na Tv.
Amesisitiza
kuwa chuo hicho kinafundisha kozi mbalimbali katika ngazi ya Cheti,
Astashahada, Shahada na Shahada ikiwemo Uhandishi wa Habari, Sheria,
Mendeleo ya Jamii, Usimamizi wa Biashara, Ualimu, Utawala, Masoko,
Utafiti, Manunuzi, Utalii, Kompyuta pamoja na uchungaji.
Maonesho
hayo yalizinduliwa Julai 27 mwaka huu katika viwanja hivyo na Baraza la
Mapinduzi na Kiongozi na Katibu Mkuu Kiongozi wa Zanzibar Mhandisi,
Zena Ahmed Said na yanatarajiwa kufikia tamati Julai 31, 2021.
No comments:
Post a Comment