HABARI MSETO (HEADER)


July 10, 2021

DANIEL CHONGOLO AWATAKA WANA CCM KUENDELEA KUIMARISHA CHAMA NA KUWALETEA WANANCHI MAENDELEO


Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Ndg Daniel Chongolo akimtwisha Ndoo Kichwani, Binti Beatrice Masasi  katika Kijiji Cha Asweketa. Kulia ni Mkuu wa Mkoa wa Songwe Mhe. Omari Mgumba mara baada ya kutembelea Mradi wa mamlaka ya Maji ya Mji Mdogo wa Vywawa wilayani mbozi.
Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Ndg Daniel Chongolo  akisaidia shuhuli ya Ujenzi wa daraja la idiwili kwenda idunda linalojengwa kwa gharamia  kiasi cha shilingi Milioni90 hadi kukamilika kwake,julai 9 2021.
Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Ndg Daniel Chongolo akitoka kukagua ujenzi wa daraja la idiwili kwenda idunda linalojengwa kwa gharamia  kiasi cha shilingi Milioni90 hadi kukamilika kwake,julai 9 2021.
Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Ndg Daniel Chongolo  akizungumza katika mkutano wa Wanchama wa Shina no5  tawi la Idogo kata ya Idiwili wilayani  Mbozi  julai 9 2021.
Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Ndg Daniel Chongolo, akigawa kadi  ya CCM kwa Mwanachama mpya  Ndg Rafael Sarawe Siwila. Kulia ni balozi wa Shina namba 2 Hasanda, Edea Samwel tonya kitongoji cha Senya, wilayani mbozi julai 9 2021.
Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Ndg Daniel Chongolo, akikabidhi kadi  ya CCM kwa Mwanachama mpya, Mteni Nzundwa Mwamlemela.
Wanachama  wa Shina no 2 zaidi ya 100 wakila kiapo mara baada ya kukabidhiwa kadi za CCM.
Mbunge wa Viti Maalum kutokea Mkoa wa Songwe, Juliana Shonza akizungumza na Wanachama na viongozi  wa shina Namba 2 lililopo katika kitongoji cha Senya, Wilayani Mbozi julai 9 2021.

Mbunge wa Jimbo la Vywawa, Joseph Hasunga  akizungumza na Wanachama na Viongozi  wa shina Namba 2 lililopo katika kitongoji cha Senya, Wilayani Mbozi julai 9 2021.

Mkuu wa Mkoa wa Songwe, Omari Mgumba akizungumza na Wanachama na Viongozi  wa shina Namba 2 lililopo katika kitongoji cha Senya, Wilayani Mbozi julai 9 2021.

Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Daniel Chongolo, akisikiliza maelezo ya Mganga mkuu wa mkoa wa Songwe Dk. Nyembea Hamadi alipotembelea maabara ya Hospitali rufaa ya mkoa inayojengwa kwa gharama za shilingi  milioni 997, wilayani mbozi julai 9 2021.
Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Ndg Daniel Chongolo akizungumza na viongozi wa serikali pamoja na watumishi wa hospitali ya rufaa ya mkoa mara baada ya kukagua maendeleo ya ujenzi wa  Hospitali rufaa ya mkoa inayojengwa kwa gharama za shilingi Bilioni 4.5  ,wilayani mbozi julai 9 2021.
Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Songwe, Elynico Mkola akipunga mkono kwa wanachama wa Shina no5  tawi la Idogo kata ya Idiwili wilayani  Mbozi  julai 9 2021.
Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Daniel Chongolo, akizungumza na Wazee wa wilaya ya Mbozi jimbo la vywawa , julai 9 2021. (Picha Zote na Fahadi Siraji CCM Blog)
 
  
Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Daniel Chongolo,  pamoja na wajumbe wengine wa Sekretarieti ya CCM Taifa  tarehe 9 Julai, 2021 ameendelea na ziara ya kuimarisha Chama Mashinani mkoani Songwe baada ya kumaliza mkoa wa Rukwa.

Katibu Mkuu akizungumza katika kikao cha mapokezi Wilayani Momba amewakumbusha wanaCCM majukumu makubwa mawili ikiwa ni kuendelea kukijenga na kukiimarisha Chama, pamoja na kufanya kazi ya kuwaletea wananchi maendeleo.

Katibu Mkuu ameongeza kuwa  kuna vyama kazi zao ni kuikumbusha CCM na kuwafanya kuwa na bidii zaidi ya kuwahudumia wananchi, hivyo wanaCCM tuendelee kutimiza jukumu letu la msingi la kuongoza nchi, na wao tuwaache watimize jukumu lao.

Akianza ziara hiyo mkoani Songwe wilaya ya Mbozi, Katibu Mkuu amefanya mikutano ya Mashina na kutembelea miradi mbalimbali ya maendeleo ikwemo mradi wa  Maji Kata ya Ihanda, Ujenzi wa Hospitali ya Mkoa wa Songwe pamoja kukagua maendeleo ya ujenzi wa Daraja la Idiwila.

Aidha, Katibu Mkuu akiwa katika mkutano wa shina namba 02 Kata ya Hasamba, amepokea wanachama wa vyama mbalimbali vya upinzani zaidi ya 100 waliohamia CCM, wakiongozwa na Ndg. Fanuel Mkisi aliyekuwa Mgombea Ubunge wa Jimbo la Vywawa kupitia CHADEMA mwaka 2020.

No comments:

Post a Comment

Pages