Katibu Mkuu Kiongozi wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, Mhe. Mhandisi Zena Ahmed Said, akikaribishwa na Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu Mzumbe, Prof. Lughano Kusiluka (Mwenye suti kushoto), alipotembelea banda la Chuo kikuu Mzumbe katika meonesho ya 16 ya Elimu ya Juu , yanayoendelea viwanja vya Mnazi Mmoja, Dar es Salaam na yatamalizika Jumamosi 31 Julai ,2021 katika viwanja vya Mnazi mmoja, Dar es Salaam.
Dkt. Thobias Mnyasenga, akitoa maelezo kwa vijana wa kidato cha sita walioonyesha nia ya kujiunga na mafunzo ya Elimu ya Juu katika Chuo Kikuu Mzumbe walipotembelea Banda la la Chuo katika Maonyesho ya Vyuo Vikuu yaliyoandaliwa na Tume ya Vyuo Vikuu Tanzania(TCU) katika Viwanja vya Mnazi mmoja jijini Dar es salaam.
Maafisa kutoka chuo kikuu Mzumbe wakitoa huduma ya udahili wa moja kwa moja kwa waombaji waliotembelea banda la Chuo Kikuu Mzumbe katika maonesho ya Vyuo Vikuu yanayoendelea katika viwanja vya Mnazi Mmoja.
Na Mwandishi Wetu
Katibu Mkuu Kiongozi wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar Mhandisi Zena Ahmed Said, ambaye ni Mgeni Rasmi katika sherehe za uzinduzi wa maonesho ya 16 ya Vyuo vikuu (TCU), yanayoendelea kwenye viwanja vya Mnazi mmoja jijini Dare es Salaam, ametembelea banda la Chuo Kikuu Mzumbe na kupongeza kazi nzuri inayofanywa na Chuo hicho.
Awali akimkaribisha mgeni rasmi kwenye Banda la Chuo hicho, Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu Mzumbe Prof. Lughano Kusiluka, amesema Chuo kimeendelea kuwa mahiri kwa kutoa elimu ya juu na hasa katika maeneo ya Utawala na Uongozi, na kufanikiwa kuzalisha viongozi wengi nchini kwa nafasi mbalimbali, akiwemo Rais wa sasa Mhe. Samia Suluhu Hassan. Amesisitiza Chuo kitaendelea kufanya vizuri zaidi chini ya uongozi wa Mkuu wa Chuo wa sasa Rais Mstaafu wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, Mhe. Dkt. Ali Mohammed Shein.
Akitoa maelezo kuhusu huduma zinazotolewa kwenye maonesho hayo, Mkurugenzi wa Mawasiliano wa chuo hicho Bi. Rose Joseph, amesema Chuo kinatoa huduma mbalimbali kwa wananchi wanaotembelea maonyesho hayo ikiwemo huduma ya ushauri wa kitaalamu kwa wanafunzi wanaotaka kujiunga kwa program mbalimbali zinazotolewa kwa mwaka wa masomo 2021/22, kufanya udahili (usajili wa moja kwa moja) kwa wanafunzi wanaojiunga na chuo hicho kuanzia ngazi ya Cheti, Stashahada, Astashada, Shahada za Awali na Shahada za Uzamili (Masters/PhD).
Huduma nyingine ni kupokea ushauri na maoni ya wateja kuhusu kuboresha program na mafunzo yanayotolewa na chuo hicho, pamoja na kuanzisha ushirikiano wa kitaaluma na vyuo mbalimbali vya ndani na nje ya nchi.
Maonyesho ya 16 ya Vyuo Vikuu nchini yamezinduliwa leo, na yataendelea hadi Jumamosi tarehe 31 Julai 2021, viwanja vya Mnazi Mmoja Dar es Salaam.
No comments:
Post a Comment