HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

July 18, 2021

KIVUMBI NA JASHO KUFUNGA VPL LEO NANI KUSALIA

 

Wachezaji wa Simba wakiwa katika mazoezi ya kujiandaa na mchezo wa kufunga pazia la Ligi Kuu Tanzania Bara dhidi ya Namungo utakaochezwa leo kwenye dimba la Taifa jijini Dar es Salaam.




Na John Marwa

Leo ndio leo hakuna cha kungoja kesho ni dakika 810 zitateseka kutamatisha Ligi Kuu Soka Tanzania Bara (TPL) Klabu 18 viwanja 9 nyasi kumenyeka.

Ni mwisho wa safari ndefu ya TPL ambapo michezo ya leo itaamua nani kusalia TPL msimu ujao huku Mwadui FC wakiwa washafungisha virago je ni Ihefu, Gwambina na JKT wataungana nae? majibu yatapatikana leo ambapo JKT Tanzania wataumana na Mtibwa Sugar katika Dimba la Azam Complex.
Mitanange mingjne Coastal Union dhidi ya Kagera Sugar mchezo mwingine wenye mvuto, Dodoma Jiji watakamuana na Young Africans, Tanzania Prisons dhidi ya Gwambina FC.

Pale Uhuru watoza ushuru wa Kinondoni KMC FC watamenyamana na Ihefu, pale Mbeya Mbeya City wanakibarua cha kutoana jasho na Biashara United kutoka Mara huku Mabatini Pwani Ruvu Shooting wakimumunya ice cream za Azam FC.

Ukiachana na mechi hizo zenye utamu wa aina yake kwa Mkapa Mabingwa wa Nchi Simba SC watakuwa wanakamilisha ratiba kwa sherehe za kukabidhiwa ubingwa mbele ya Namungo FC.

Tayari timu nne za juu zimeshajulikana Simba, Yanga, Azam na Biashara United. Huku Mwadui akiwa admini wa kundi za Klabu zinazoshuka daraja je ni Ihefu, Gwambina na JKT ama ni Mtibwa Mbeya City??

Hakika ulikuwa msimu bora sana kuutazama acha muda usogee tuutamatishe msimu kwa burudani mujarabu.kwa heri VPL karibu TPL.

No comments:

Post a Comment

Pages