●Makamu wa Rais aweka jiwe la Msingi
●Udahili kuongezeka kutoka 400 hadi 800
Ameyasema
hayo wilayani Kasulu mkoani Kigoma wakati wa kuweka jiwe la Msingi la
ujenzi wa majengo mapya ya Chuo hicho ambapo amewataka walimu tarajali
kusoma kwa bidii kwa kuwa sasa miundombinu imeboreshwa.
Makamu wa Rais amesema ameridhishwa na taarifa Ujenzi huo kwa kuwa umezingatia
matumizi Bora ya Nishati mbadala na nafuu na pia uhifadhi wa mazingira.
Aidha amesema ni vizuri chuo hicho kikachukua tahadhari zote za kuzuia
majanga yakiwemo ya moto na kuwataka walimu tarajali wa Chuo cha Ualimu
Kabanga watakaohamia katika majengo mapya ya Chuo hicho kutunza
miundombinu hiyo ili iweze kutumika kwa muda mrefu.
Pia
ameishukuru Serikali ya Canada kwa kuwezesha ujenzi wa majengo hayo
mapya ya Chuo cha Ualimu na Vyuo vingine vya Ualimu nchini.
"Serikali
ya Rais wetu Samia Suluhu Hassan inathamini urafiki wa muda mrefu
na ndugu zetu wa Canada, nakuomba Mhe. Balozi kupitia kwako utupelekee
salamu zetu kwa Waziri Mkuu wa Canada kutoka kwa Watanzania,
tunaishukuru serikali yake pamoja na wananchi kwa kuendelea kushirikiana
nasi tunapofanya jitihada za kujikomboa kielimu na katika maeneo
mengine ya nchi yetu Canada imekuwa mbia muhimu," amesema Makamu wa
Rais
Kwa upande wake Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof.
Joyce Ndalichako amesema Mradi huo mpaka utakapokamilika utagharimu
zaidi ya Shilingi Bilioni 11 na kwamba umefadhiliwa na Serikali ya
Canada kupitia Programu ya Kuimarisha Elimu ya Ualimu (TESP).
Ndalichako
amesema mradi huo utakapokamilika utaongeza idadi ya Wanachuo kutoka
400 hadi 800 na utakuwa na miundombinu yote na vifaa vyote vya
kufundishia na kujifunzia.
Aliongeza kuwa kwa upande wa Sekta ya
Elimu, Serikali ya Canada imekuwa ikifadhili miradi mbalimbali na
kushirikiana nao kwenye masuala yanayohitaji ushauri wa kitaalamu
hususani kwenye mambo ya elimu ya ualimu ambapo programu ya TESP ambayo
ni ya Miaka 7 ina thamani ya jumla ya dola za Canada milioni 53 ambazo
ni sawa na zaidi ya shilingi bilioni 90 za Tanzania.
Nae balozi
wa Canada nchini Tanzania Pamela O'donnel amesema Canada inayofuraha
kushirikiana na Serikali ya Tanzania katika juhudi za kuboresha mfumo wa
ufundishaji kwa faida ya watoto wa kitanzania
Amesema ujenzi wa
Chuo cha Ualimu Kabanga ni wa kisasa unaozingatia mbinu za kimazingira
na hivyo kuwa na nafasi kubwa ya kuchangia juhudi za Serikali za
kukabiliana changamoto ya mabadiliko ya tabia nchi. Pia itachangia
jitihada za maendeleo endelevu ambayo ni nishati safi usawa wa kijinsi
na kupambana na madiliko ya tabia nchi na hivyo kukifanya Chuo hicho
kuwa cha karne.
Balozi O'dennel ameongeza Canada ni moja ya nchi
ya kwanza duniani kupitisha sera ya nchi yenye kuzingatia usawa wa
kijinsia na kwamba anafarijika kuona mradi unahakikisha wakufunzi
wasimamizi wa elimu na mifumo yote inazingatia usawa wa kijinsia na
kwamba Serikali yake iko tayari kuendelea kushirikiana na Tanzania
kuimarisha Sekta ya Elimu Hususan Elimu ya Ualimu.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip Mpango akiweka jengo na Msingi katika majengo mapya ya Chuo cha Ualimu Kabanga-Kasulu, Kigoma. Kulia ni Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Prof. Joyce Ndalichako na Balozi wa Canada nchini Tanzania,.Pamela O'donnel. Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Philip Mpango amesema ujenzi wa majengo mapya ya Chuo cha Ualimu Kabanga ni moja ya mikakati ya Serikali kuboresha mazingira ya utoaji wa elimu ya nchini.
No comments:
Post a Comment