HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

July 13, 2021

Maafisa uvuvi waonywa kuwabambikizia kesi wavuvi


Na Lydia Lugakila, Muleba


Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Mashimba Mashauri Ndaki
ameagiza maafisa uvuvi Wilayani Muleba kutumia Sheria na taratibu ili kuepuka kuwaonea au kuwabambikizia kesi wavuvi wanaofanya shughuli za uvuvi katika ziwa Victoria wakati wa kudhibiti vitendo vya uvuvi usiokubalika kisheria.

Agizo hilo kwa waziri wa mifugo na uvuvi limebainika  wakati wa ziara ya kikazi mkoani Kagera wakati akizungumza na watumishi wa halimashauri ya Wilaya ya Muleba ambapo ameeleza  kuwa amekuwa akipata malalamiko kutoka kwa wavuvi ikiwemo kuvunjiwa vifaa vya ikiwemo mitumbwi na kuchomewa nyavu zao.

" Kitendo cha kuwaonea wavuvi kwa kuwabambikizia kesi kinapunguza nguvu kazi ya utendaji kazi zao za uvuvi, hivyo basi naagiza kutumia sheria na taratibu za Serikali wakati wa kudhibiti vitendo vya uvuvi usiokubalika kisheria katika ziwa victoria.
 alisema waziri Ndaki".

Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya Muleba  Toba Nguvila Wilaya hiyo inahitaji maafisa mifugo na uvuvi kwa ajili ya kutoa elimu na kudhibiti vitendo vya uvuvi usiokubalika kisheria,kwani kwa sasa kuna Jumla ya watumishi wa idara ya mifugo na uvuvi wapatao 35 na wanaohitajika ni zaidi ya 200.


Naye Katibu tawala Mkoa wa Kagera profesa Faustin Kamuzola ameiomba Wizara hiyo ya Mifugo na uvuvi kuwapatia vitendea kazi watumishi wa halmashauri hiyo, ikiwemo pikipiki kwa ajili ya kurahisisha majukumu yao.

Hata hivyo kwa upande wake katibu Mkuu wa Wizara ya mifugo na uvui Profesa Elisante Ole Gabriel amesema tayari Wizara hiyo imeomba kibali kwa ajili ya kuajiri  watumishi wapya  na mwaka huu wa fedha wa 2021/2022 inatarajia kugawa Jumla ya pikipiki 500 ili kuwandolea watumishi hao adha wanayoipata kwa Sasa.

No comments:

Post a Comment

Pages