HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

July 13, 2021

MBUNGE BUKOBA VIJIJINI ATOA MILIONI 27 KWA VIJIJI 20


 

Mbunge wa jimbo la Bukoba vijiji Dkt. Jasson Samson Rweikiza akitoa ahadi yake kwa wananchi.



Na Lydia Lugakila, Bukoba


Mbunge wa Bukoba Vijijini Dkt. Jasson Rweikiza ameanza kutekeleza ahadi yake ya kutoa shilingi milioni 27 kwa vijiji 20 vilivyoongoza kwa kura wakati wa uchaguzi mkuu mwaka jana

Akizungumza na wananchi wa Kata Mikoni ambayo imeingiza vijiji vinne katika vijiji 20 vilivyoongoza, Dkt Rweikiza ametoa shilingi milioni 5 kwa kijiji cha Kagondo kilichoshika nafasi ya kwanza huku vijiji vingine vitatu vikipata milioni moja kila kimoja hivyo vijiji vyote kuchukua milioni 8.

Akizungumza kwa niaba ya wananchi,diwani wa kata hiyo Sadoki Ijunga amemshukuru mbunge huyo huku akibainisha kuwa fedha hizo wananchi wao wenyewe ndiyo watazipangia matumizi.

No comments:

Post a Comment

Pages