HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

July 13, 2021

WAZALISHAJI MAZAO YA VIUNGO WATAKIWA KUZALISHA BIDHAA ZENYE VIWANGO

 Na Asha Mwakyonde, Dar es Salaam

WAZALISHAJI wa mazao ya viungo nchini wametakiwa kuhakikisha bidhaa wanazozalisha zinakidhi viwango kwa lengo la kupata soko la ndani na nje ya nchi ambalo  litawaongezea thamani ya bidhaa zao.

Hayo yamesema na Naibu  Waziri wa Viwanda na Biashara, Exaud Kigahe Jijini Dar es salaam wakati uzinduzi wa  nembo  ya viungo Tanzania katika Maonyesho ya 45 ya Biashara ya Kimataifa (DITF) yanayoendelea katika viwanja vya Mwalimu Julias Nyerere.

Amesema maendeleo ili kuyafikiwa lazina kuwe  bidhaa bora hivyo ni muhimu wazalishaji kuzingatia viwango vya ubora vinavyotakakiwa kwa lengo la kukuza masoko.

"Nchi ya Tanzania ni miongoni mwa nchi inayozalisha kwa wingi bidhaa za viungo na hivyo  uwepo wa nembo ya alama ya viungo Tanzania utasaidia bidhaa hizi kutambulika ndani na nje ya nch," amesemai.

"Ameongeza kuwa uwepo wa nembo katika bidhaa za viungo utasaidia kukuza soko kwa kiasi kikubwa na  bidhaa kutambulika ndani ya nchi na nje sambamva na  kuweka imani kwa wanunuzi wa bidhaa za viungo"amesema

Kigahe amesema lengo la Serikali ni kuhakikisha wanadhibiti upotevu wa mazao baada ya kuvunwa ambapo Serikali inatarajia kuongeza Viwanda vya kuchakata mazao ya viungo kama vile tangawizi.

Kwa upande wake Mkurugenzi Mkuu wa kituo cha kimataifa cha biashara ( MARKUP) Safari Fungo amesema uwepo wa nembo katika bidhaa za viungo utasaidia kuitangaza nchi katika bidhaa zinazotoka nchini na kuziongezea thamani.

Amesema sasa wakati umefika kwa wa kutagaza bidhaa zinazozalishwa hivyo ni muhimu wazalishaji kutambua umuhimu wa nembo viungo Tanzania katika bidhaa zao.

Naye Balozi mteule ambaye pia ni Mkurungezi Mtendaji wa Mamlaka ya Maendeleo ya biashara (Tantrade) Edwin Rutageruka amesema nembo ya viungo ya Tanzania itasaidia kuitagaza nchi pamoja na kuwasaidia Wafanyabiashara kutambulika kuaminiwa .

No comments:

Post a Comment

Pages