HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

July 06, 2021

Mbunifu VB alia na soko la ngozi

Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Prof. Joyce Ndalichako, akipata maelezo kutoka kwa mbunifu wa dawa ya kuongeza thamani ya biadhaa ya ngozi VB, Dk. Never Mwambela, alipotembelea banda la COSTECH kwenye Maonyesho ya 45 ya Biashara ya Kimataifa Dar es Salaam (DITF).


 Na Selemani Msuya

 

MBUNIFU wa dawa ya kuongeza thamani ya biadhaa ya ngozi VB, Dk. Never Mwambela amesema pamoja na kupatikana kwa dawa hiyo bado kuna changamoto ya  soko ya bidhaa hiyo.

Mwambela ambaye ni Muhadhiri Mwandamizi katika Chuo cha Usimamizi wa Wanyamapori Mweka, alisema hayo jana wakati akizungumza kwenye Maonyesho ya 45 ya Biashara ya Kimataifa Dar es Salaam (DITF) maarufu Sabasaba yenye kauli mbiu ' Uchumu kwa Ajira na Biashara Endelevu'  yanayofanyika katika Viwanja vya Julius Nyerere Temeke jijini Dar es Salaam.

Alisema bidhaa ya ngozi katika nchi ya Tanzania inapatikana kila mahali ila changamoto kubwa ni soko pamoja na kwamba wameweza kufikia wafugaji 400 na kuwapatia dawa ya kuongeza thamani bidhaa hiyo.

“Nimeweza kubuni bidhaa aina ya VB ambayo inaweza kuongeza thamani kwenye ngozi ili isikose soko lakini katika hali ambayo sikutarajia nimekuta nafanikiwa kutibu ngozi ila soko limekuwa adimu,” alisema.

Alisema alifanikiwa kufadhaliwa na Tume ya Sayansi na Teknolojia (COSTECH) kwa kuwezesha shilingi milioni 70 ambapo alifikia wafugaji 400  na kwa sasa zipo ngozi zaidi ya 10,000 hazina ssko hivyo wanaoomba wanunuzi wa ngozi wajitokeze.

Mbunifu huyo alisema mradi umeonesha matokeo chanya kwa kutibu ngozi hivyo anaomba wenye viwanda vya ngozi kujitokeza kununua bidhaa hiyo ili waitumie.

Mwambela alisema kiasi hicho cha ngozi 10,000 kinapatikana katika wilaya nne za Mkoa wa Arusha ambazo ni Longido, Monduli, Arumeru na Arusha yenyewe.

“Naomba Serikali kupitia COSTECH wawezeshe wafugaji katika maeneo yao mashine ambazo zitachakata na kutengeneza bidhaa katika ngazi ya vijiji, kata, tarafa, wilaya na mkoa,” alisema.

Alisema viwanda hivyo vitaweza kutekeleza kuali mbiu ya maonesho ya sabasaba ambayo inasema Uchumu kwa Ajira na Biashara Endelevu'.

Akizungumzia kilio hicho Mkurugenzi wa COSTECH, Dk. Amos Nungu alisema changamoto zote ambazo watafiti na wabunifu wanapitia wanatarajia kukaa pamoja na kujadili namna ya kuzitatua.

“Sisi hawa ndio watu tunawataka hivyo nikuahidi kuwa tutakaa nao na kuwasilikiliza ili tujue ni eneo lipi linapaswa kupewa msukumo zaidi na kufanikisha mchakato mzima,” alisema.

No comments:

Post a Comment

Pages