HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

July 07, 2021

Mhandisi Sangweni: Kuna changomoto za wataalamu usimamizi wa uchimbaji gesi asilia



 Kaimu Mkurugenzi wa Mamlaka   ya Udhibiti  wa Mkondo wa Juu wa Petroli(PURA), Mhandisi  Charles  Sangweni  akizungumza na waandishi wa habari.

 

Na Asha Mwakyonde, Dar es Salaam

KAIMU Mkurugenzi wa Mamlaka   ya Udhibiti  wa Mkondo wa Juu wa Petroli(PURA), Mhandisi  Charles  Sangweni  amesema bado kuna changamoto ya nafasi  muhumu za utafutaji mafuta na gesi asilia ambazo  zinashikiliwa na wageni.

Mhandisi Sangweni amesema  nafasi ya mtu anayesimamia uchimbaji ,anayeongoza kila kitu hakuna Mtanzania hata mmoja anayeshika nafasi hiyo.

Akizungumza jana katika  banda  lao  la maonyesho ya 45 ya Kimataifa ya Biashara ya Dar es Salaam (DITF), yanayoendele kufanyika katika viwanja vya Mwalimu Nyerere yenye kaulimbiu ya  ' Uchumi wa Viwanda Ajira kwa Vijana  na Biashara Endelevu'

Amesema wana mfano miwili kipindi cha nyuma  walichimba  visima  waliokuwa na wafanya ndani ya meli  kama 160 lakini Watanzania walikuwa wanane tu.

" Tulipofika wakaimarisha mwaka 2018 tulichimba kisima kilichokuwa kimepewa jina la Pilibpili  One  tulikuwa Watanzania 58, naamini leo hii ikitokea kazi yoyote Watanzania wataongeza," amesema Mhandisi huyo.


Mhandisi Sangweni ameongeza kuwa kwa sasa wanashughuli zinazoendelea  maeneo ya Ruvu  na kwamba wanatimu ya watu zaidi ya 300 lakini changamoto iliyopo ni moja ya zile nafasi muhimu bado zinashikiliwa na wageni.

Amesema wanajua kwamba muda unavyoendelea Watanzania Wanazidi kujifunza kupitia wageni  hao na mwisho wa siku watapata wenye nafasi hiyo.

Mhandisi huyo amesema fursa zilizopo kwenye mkondo wa juu wao ndio wanasimamia  na kwamba Kuna sheria, miongozo, kanuni lakini hazitoshi kama hawataungana na yule anayesimamia.

Ameongeza kuwa rasilimali  za  hapa nchini ni za Watanzania na katiba imeelekeza wazi rasilimali yoyote ni ya mtanzania alieelewa haki yake ni kumiliki ardhi.

Mhandisi huyo ameeleza kuwa kwenye shushuli za utafutaji  wa mafuta na gesi asilia wanapokuwa na uchimbaji wa visima wanakuwa na fursa nyingi kama vile za chakula, usafirishaji, mawasiliano ni sehemu ambayo hata mtu binafisi asiye na kampuni  anapata fursa hiyo..

Katika hatua nyingine mahandisi huyo amesema hadi sasa Mamlaka yao imeingia mikataba takribani Makampuni 11 kati ya hayo Makampuni matatu yapo katika uzalishaji wa mafuta na gesi asilia.

Pia amesema katika Makampuni hayo  11 kampuni moja ni la wazawa wa ya kitanzania ambao yanawekeza katika uzalishaji wa sekta hiyo ya mafuta na gesi asilia.

Mhandisi Sangweni amesema mwaka 2010,Pura ilifikia hadi Makampuni  27 lakini ilipofika mwaka 2014 bei ya mafuta ilishuka sana  huku Makampuni mengi yaliondoka.

Ameeleza kuwa   kila mkataba unaoingia na PURA, ni lazima TPDC iipitie kwani  ni mbia hivyo uzawa wao unadhibitisha kupitia TPDC.

No comments:

Post a Comment

Pages