HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

July 07, 2021

WAFANYABIASHARA WATAKIWA KUTUMIA DUKA MTANDAO

 Asha Mwakyonde, Dar es Salaam

WAZIRI  wa Habari,  Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia  Dkt. Fautine Ndugulile amewataka wafanyabiashara, wajasiriamali na wenye viwanda kutumia mfumo wa duka mtandao ili kuuza na kununua bidhaa zao popote walipo

Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania na Shirika la Posta Tanzania waUendeshaji wa Duka Mtandao


Hayo aliyasema jana wakati akizindua mfumo huo katika  maonyesho ya 45 ya Kimataifa ya Biashara ya Dar es Salaam (DITF), yanayoendele kufanyika katika viwanja vya Mwalimu Nyerere yenye kaulimbiu ya  ' Uchumi wa Viwanda Ajira kwa Vijana  na Biashara Endelevu" wakati wa Uzinduzi wa Ushirikiano wa Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania na Shirika la Pasta Tanzanian wa Duka Mtandao (e_sjop).


'Dkt Ngugulile amesema katika mtandao huo mfanyabiashara atapata fursa ya kununua na biashara  zao.

Amesema Kazi yao  ni kuunganisha masuala ya habari na tekenolojia na kwamba Wizara hiyo imeanzishwa mahsusi kuhakikisha masuala mbalimbali ya kijamii yanaendelea.

" Huku mbele tunapokwenda matumizi ya tehama yatakuwa makubwa kutokana na  Sayansi na Teknolojia  hasa kwa upande wa Mawasiliano.

"tunakwenda kufungua milango ya masoko na mauzo kwa wajasirimali kuuza biashara zao popote," amesema.

Ameongeza kuwa hiyo ni  fursa hapa nchini kwa wenye viwanda na watu wetu wajasiriamali kutumia duka mtandaoni popote alipo.


'Tunataka kuwa na posta ya kidigitali, tunajikita na huduma nyingine tumenunua magari matano na tutaongeza mengine ili kuweza kusafirisha kwa wakati.

Aidha ameeleza kuwa wanakuja na sheria ambayo inaenda kusimamia taarifa binafisi.


Kwa upande wake  Waziri wa Viwanda na Biashara Prof. Kitila Mkumbo amesema kuwa tukio hilo linaimarisha ushirikiano hilo ni jamabo jema linaelekeza watu wafanye kazi kwa pamoja.


"Hapa tunaenda kunganisha wafanyabiashara na makapuni, mtu anaweza akawa na mambo makubwa bila kuwa na kibanda.," amesema Prof. Kitila.

No comments:

Post a Comment

Pages