Jeshi
la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam limewatahadharisha vijana ambao
ni wahalifu waishio kwenye viunga vya Mkoa huo kuachana na matendo hayo
na kwamba Jeshi hilo litahakikisha wanawakamata na kuwachukulia hatua
za kisheria wale wote watakaobaika kutenda makosa hayo.
Hayo
yameelezwa na kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam ACP
Muliro Jumanne wakati akiongea na Waandishi wa habari kwenye Ukumbi
uliopo Makao Makuu ya Polisi Dar es Salaam.
Kamanda
Muliro amesema vitendo vya uporaji imekua ni kero kubwa Jijini Dar es
Salaam na kutoa onyo Kali Kwa vijana wote wanaofanya vitendo hivyo.
Kamanda
Murilo alisema kwenye operesheni ya kupambana na vitendo vya uporaji na
uvunjaji wa nyumba wameweza kukamata mali za Simu,TV,Laptop n.k
zilizoibiwa katika maeneo mbalimbali ya Mkoa huo
Katika
hatua nyingine Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam imekamata
Silaha mbili aina ya Bastola na hii ni kutokana na ushirikiano mzuri
baina ya wananchi na Jeshi Hilo
Sambamba
na hilo alitumia wasaaa huo kuwapongeza Wannachi kwa mashirikiano
makubwa wanayoyatoa ili kuhakikisha vitendo vya uhalifu vinadhibitiwa na
kuondoka katika Mkoa huo
Alisisitiza
kuwa Jeshi la Polisi linaendelea na operesheni mbalimbali katika
kuhakikisha wanadhibiti matukio ya uhalifu na uvunjaji wa sheria za Nchi
No comments:
Post a Comment