Kampuni
ya Bia ya Serengenti (SBL) imezindua Kampeni ya Tunyayuke Pamoja na
kubainisha kuwa kupitia kampeni hiyo itatoa Sh Bilioni 2.3 kwa ajili ya
kukabiliana na Ugonjwa wa Corona (Covvid-19).
Akizugumza katika uzinduzi wa kampeni hiyo leo jijini Dar es Salaam
Mkurugenzi
Mtendaji wa SBL Mark Occiti amesema kampeni itawalenga wamiliki wa
baa,wateja na wafanyakazi wa baa na kwamba fedha hizo zitatumika katika
tahadhari ya ugonjwa huo kwa kuweka sehemu za kunawia mikono, vitakasa
mikono, viti na maturubai kwa baa zote zitakazopata nafasi.
Amebainisha
kuwa kampeni hiyo itazilenga baa 2000 katika mikoa mitatu ikiwemo Dar
es Salaam, Arusha na Zanzibar na kwamba kuna vigezo vitatumika ili baa
ipate fursa ya kuingia kwenye kampeni hiyo.
Amesisitiza
kuwa kampeni hiyo itasaidia wamiki hao na wafanyakazi na wateja wao
kujihadhari na ugonjwa huo kwani watatakiwa kuzingatia kanuni za usafi
zitakazowekwa katika maeneo ya baa.
Mkurugenzi
huyo amesema SBL imezindua kampeni ikiwa ni mwendelezo wa kampuni hiyo
kukabiliana na ugonjwa huo na kwamba mwaka jana walitoa vitakasa mikono,
vipeperushi vya kutoa elimu ya Corona kwa umma.
Aidha
amesema kampeni hiyo itasaidia kuwainua kimauzo wateja wao kwani mwaka
jana hali ya biashara ilikuwa mbaya kutokana na ugonjwa huo hivyo
wanaamini wamiliki watachangamkia fursa hiyo kwa kujisajili.
Kwa
upande wake Mkurugenzi wa Mahusiano wa kampuni hiyo John Wayancha
amesema wamiliki wa baa watatakiwa kujisajili katika mtandao wa SBL ili
wapate baada kukidhi vigezo vilivyowekwa ikiwemo ukubwa wa baa na uwepo
baa mwaka mmoja kabla ya Corona.
Amesema kuwa
mpango kampeni hiyo ni ya miaka 2 na kwamba imelenga mikoa hiyo kutokana
na kuwa hatari ya maambukizi ya Corona sababu ya mwingiliano wa watu
hasahasa wageni wanaoingia mikoani humo.
Naye
Msambazaji wa Bia za SBL, Kevin Tegwa ameipongeza na kuishukuru kampuni
hiyo kwani inaonyesha jinsi inavyowajali wateja wake katika kuwasaidia
kujihadhari na ugonjwa huku wakiendelea na shughuli zao.
Mfanyabiashara
Mramba amesema mwaka jana mauzo yalidorora kutoka na watu kuhofia
ugonjwa na kwamba kupitia kampeni hiyo anaamini watafanya biashara
katika mazingira salama.
No comments:
Post a Comment