Mmoja wa wanafunzi walioshiriki katika kubuni maabara hiyo, Hawa Kindamba akielezea hadibini kitaalamu Micro Scope inavyotumika kuona vitu vidogo vidogo ambavyo havionekani kwa macho.
Na Asha Mwakyonde, Dar es Salaam
CHUO cha Mafunzo ya Ufundi Stadi(VETA), Chang'ombe kimebuni Maabara ya kutembea aina ya gari ambayo tayari imeshapewa kibali cha kutumika katika shule za sekondari na msingi.
Maabara hiyo ina huduma za mafunzo kwa vitendo zaidi kuhusu masomo ya Sayansi ikiwamo Fizikia
Akizungumza ndani ya Banda la Mamlaka ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi Stadi (VETA) kwenye maonyesho ya 45 ya Kimataifa ya Biashara ya Dar es Salaam(DITF) maarufu kama sabasaba yaliyoanza Juni 28 mwaka huu, Mwalimu wa VETA Chang'ombe, Emmanuel Bakula ameseema maabara hiyo itakuwa inafanya kazi katika shule za sekondari na msingi zenye uhaba wa maabara hiyo.
Amesema maabara hyo imetengenezwa mwaka jana na kwqmba mwaka huu ikapelekwa kwenye Maonyesho ya Mashindano ya Kisayansi, Teknolojia na Ubunifu(MAKISATU), na kushinda ambapo imepata nafasi ya kwanza katika mashindano hayo.
"Maabara hii ko tayari kwa matumizi pia inaweza kwenda mahali popote itakapohitajika hasa kwa shule ambazo zina uhitaji na siziso na maabara au zenye maabara lakini hazina vifaa kwani maabara hii inavifaa vyote vinavyohitajika katika maabara,"amesema.Bakula.
"Na unaweza kuinunua kabisa na vifaa vyake ndani, pia huwa inakuwa na wataalam wetu ambao ukiwahitaji wanafika popote kwa ajili ya kuwafundisha wanafunzi kupitia hii maabara,"ameeleza Bakula.
Kwa upande wake mmoja wa wanafunzi walioshiriki katika kubuni maabara hiyo, Hawa Kindamba, amesema ubunifu huo utasaidia changamoto ya baadhi ya wanafunzi kutopenda masomo ya sayansi kutokana ukosefu wa maabara.
Pia, amewashauri wanafunzi wa kike kupenda masomo ya sayansi kwa kuwa hayana ugumu wowote.
No comments:
Post a Comment