Na Jasmine Shamwepu, Dodoma
SERIKALI kupitia Wizara ya Afya imewaita kazini watumishi wa Umma katika kada ya Afya wapatao 473 wakiwemo Madaktari Bingwa,Wauguzi na Wataalam wa mionzi kutokana na kukidhi vigezo vya ajira.
Hayo yameelezwa leo Jijini Dodoma na Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Profesa Abel Makubi wakati akizungumza na waandishi wa habari kuhusiana na ajira hizo.
Profesa Makubi amesema watumishi hao waliochaguliwa ni kutokana na kujaza nafasi zilizoachwa wazi na watumishi wa kada mbalimbali katika Sekta hiyo ambao walifikia ukomo wa utumishi ikiwemo kustaafu,kufariki na wengine kuacha kazi.
Hata hivyo amefafanua kuwa jumla ya nafasi 473 zilitangazwa na Wizara ya Afya kupitia tovuti ya Wizara mnamo Mwezi mei mwaka huu na walipokea jumla ya maobi 19757 kati ya hayo maombi4760hawakukamilisha kujaza maombi yao na hivyo kutokidhi vigezo huku maombi9338 yakiwa yamekidhi vigezo vya kuajiriwa.
Katika hatua nyingine Katibu Mkuu huyo amewataka waliochaguliwa katika nafasi hizo kuripoti katika Hospitali ya Mirembe Jijini Dodoma kuanzia leo hadi Julai9 Mwaka huu wakiwa na nakala halisi pamoja na vivuli vya vyeti yao.
Pia Katibu Mkuu huyo ametoa wito kwa waombaji wote wa nafasi za ajira kuhakikisha wanakuwa makini katika kujaza fomu za maombi ya kazi ili kukidhi vigezo.
July 06, 2021
Home
Unlabelled
Serikali yawaita kazini watumishi 473 kada ya Afya.
Serikali yawaita kazini watumishi 473 kada ya Afya.
Share This
About HABARI MSETO
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Author Details
Ut wisi enim ad minim veniam, quis nostrud exerci tation ullamcorper suscipit lobortis nisl ut aliquip ex ea commodo consequat. Duis autem vel eum iriure dolor in hendrerit in vulputate velit esse molestie consequat.
No comments:
Post a Comment