Mabingwa wa Ligi Kuu ya Soka Tanzania Bara, Simba SC wakifurahia ubingwa wao baada ya kukabidhiwa kombe katika mchezo wa kufunga pazia ya dhidi ya Namungo FC uliofanyika kwenye Uwanja wa Mkapa na kuibuka na ushindi wa bao 4-0.
Na John Marwa
YAMETIMIA, Mabingwa wa Nchi Simba SC wamekabidhiwa taji la nne mtawalia la Ligi Kuu Soka Tanzania Bara TPL msimu wa 2020/21 uliotamatika leo.
Simba wemenogesha sherehe za kukabidhiwa Ubingwa kwa kuwachalaza Namungo FC kwa mabao 4-0, mabao ya Chris Mugalu mawili, Medie Kagere moja na John Bocco Captain fantastic bao moja.
Kwa ushidi huo Simba wamekamilisha michezo 34 kwa kujikusanyia point 83 huku wakifunga mabao 78 na kuruhusu 14.
Simba wamekabidhiwa kombe lao na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Amos Makala akiknhozana na Mtendaji Mkuu wa Bodi ya Ligi Kuu Soka Tanzania Bara TPLB, Almas Kasongo sambamba na Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Simba Mohamed Dewji.
Wakati Simba wakikabidhiwa Ubingwa Klabu nyingine zimetamatisha TPL msimu wa 2020/21 Yanga wamemaliza kwa suluhu dhidi ya Dodoma Jiji FC, kwa MATOKEO hayo Yanga wanamaliza nafasi ya pili Azam FC nafasi ya tatu na Biashara United nafasi ya nne.
Kwa upande wa timu zilizoshuka daraja JKT Tanzania, Ihefu FC na Gwambina FC wameungana na Mwadui FC kusepa TPL msimu ujao na sasa maisha yao yanahamia Ligi Daraja la Kwanza FDL.
Wakati Klabu nne zikishuka Daraja Wagosi wa Kaya na Mtibwa Sugar wao wana michezo ya kujiuliza katika mitanange ya pay off dhidi ya Trans Camp na Pamba, ambapo Pamba watamenyana na Coastal Union na Trans Camp wakionyeshana umwamba.
TPL imemalizika kobabe kwa wekundu wa Msimbazi kutoa mfungaji bora kwa msimu wa nne mfululizo ambapo John Bocco Captain fantastic ametwaa kiatu cha Mfungaji bora kwa kutikisa nyavu mara 16.
No comments:
Post a Comment