Na Asha Mwakyonde, Dar es Salaam
MKURUGENZI wa Jumuiya ya Wafanyabiashara Wanawake Tanzania (TABWA), Noreen Mawalla ameiomba Serikali kuwashika mkono kwa kuwajengea maeneo ya kuzalishia bidhaa zao.
Hayo amesema jana jijini Dar Dar es Salaam katika viwanja vya Mwalimu Nyerere wakati akifunguzi rasmi wa Maonesho ya 45 ya Kimataifa ya Biashara ya Dar es Salaam maarufu Sabasaba, amesema serikali inaweza kujenga sehemu ya kuzalishia ili mwanamke auze bidhaa zake kokote pale.
Mawalla amesem kuwa wamekuwa wakiwafundisha Wanawake masuala ya ujasiriamali lakini wanazalisha katika maeneo yao ya nyumbani ambako hakuna vigezo vinavyohitajika na ambapo si salama kwa afya ya mlaji.
" Serikali inaweza kujengea maeneo maalumu wanawake wakawa wanaenda kuzalisha bidhaa zao na kila kitu kikafanyika huko huko na hii itamsaidia kupata masoka ndani na nje," amesema Mkurugenzi huyo.
Amesema wanawake wengi ni wajasiriamali lakini tatizo lao ni maeneo ya kufanyia biashara zao na sehemu ya kuzalishia kwa wale wanaozaliwa.
"Tunamshukuru Rais wa awamu ya sita mama yetu Samia Suluhu Hassan anatilia mkazo masuala ya kiuchumi kwa mwanamke hata katika mkutano wake nchini Ufaransa alichagua eneo la wanawake katika uchumi," amesema.
Akizungumzia maonyesho amesema wanawake wajitokeza kushiriki Maonyesho hayo na kutaja badadhi ya mikoa kuwa ni Dar es Salaam, Iringa,Mbeya,Arusha, Morogoro,Kilimanjaro,Kagera,Dodoma,Pwani na Zanzibar.
Ameongeza kuwa Jumuiya hiyo pia imewapokea wafanyabiashara kutoka nchi ya Burundi na kwamba wameyafurahia maonyesho hayo.
Kwa upande wake mmoja wa wafanyabiashara kutoka Burundi Ndihokuvwayo Jackson amesema kuwa hii ni mara ya Saba kushiriki maonyesho hayo
No comments:
Post a Comment