Mkuu wa Takukuru Mkoa wa Pwani Suzan Raymond akizungumza
na waandishi wa habari kuhusiana na wimbi la baadhi ya watu ambao
wanajifanya maafisa wa Takukuru.
NA VICTOR MASANGU, PWANI
TAASISI
ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) Mkoani Pwani imewataka
wananchi kuchukua tahadhari dhidi ya matapeli wanaojifanya ni maofisa wa
Taasisi hiyo ili waweze kuchukuliana hatua Kali za kisheria.
Mkuu
wa Takukuru Mkoa wa Pwani Suzana Raymond ametoa tahadhari hiyo akitoa
taarifa ya utendaji kazi wa miezi mitatu kwa waandishi wa habari.
Suzana
alisema wapo wanachi wamekuwa wakipigiwa simu na watu wanaodaiwa kuwa
ni matapeli wakitakiwa kufika kwenye ofisi za TAKUKURU na wanapofika
hapo hakuna taarifa za wito wao.
Aidha
Suzana ameongeza kuwa katika kipindi cha miezi mitatu kutoka April
hadi June wamepokea malalamiko 127 kati ya hayo 57 uchunguzi wake
unaendelea na 70 hayahusiani na Taasisi hiyo.
Alisema
katika kipindi hicho kesi 15 ziliendelea kuendeshwa katika mahakama
mbalimbali za mkoa wa Pwani na kwa miezi hiyo mitatu kesi sita
zilitolewa maamuzi na Jamhuri ilishinda na washitakiwa walitakiwa kulipa
faini au kutumikia kifungo.
Pia katika hatua nyingine aliwahimiza wananchi wote wa mkoa wa Pwani
kuhakikisha wanawafichua watu wote ambao wanavunja Sheria kwa kujifanya
wao ni watumishi wa Takukuru.
No comments:
Post a Comment