Na Mwandishi Wetu
WANAWAKE wawili wanaokutoka familia ya Marehemu Amiri Mrisho wa Dar es Salaam wamemlilia Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan kuingilia kati mgogoro wa ardhi yao, waliyoachiwa na mume wao aliyefariki 2006.
Wajane hao ambao ni Anseline Mrisho na Amina Mrisho wamedai mchakato wa kuuzwa kwa kiwanja hicho ni wa kitapeli kwa kuwa baada ya kufariki mume wao hakuna kikao cha familia ambacho kilikaa kujadili kuuza eneo hilo au kuugawana mirathi.
Eneo hilo la kiwanja namba 108 post Access kilichopo eneo la Mapambano Wilaya ya Temeke, Dar es Salaam limekuwa na mgogoro kwa takribani miaka 15, baada ya mmoja wa watoto wa Marehemu, Sophia Mrisho kudaiwa kuliuza kinyemela kwa Kampuni ya Nahla Development.
Kwa mujibu wa Anseline Mrisho, Mjane wa Marehemu Mrisho, amesema mtoto huyo ambaye amegeuka kuwa msaliti wa familia, alifungua kesi ya kudai mirathi namba 167 ya mwaka 2006 katika Mahakama ya Mwanzo Kariakoo.
Aidha Mchakato wa kuuzwa kwa kiwanja hicho ni wa kihuni kwani baada ya kufariki Mzee Mrisho hakuna kikao cha familia kilichokaa na kujadili kuuza eneo hilo wala kugawana mirathi.
“Sisi tunamlilia Rais Samia, Rais wetu wajane na Rais wa wanyonge kuwa tumeporwa eneo letu na Kampuni ya NAHLA Development, eneo hilo tunalimiliki kwa zaidi ya miaka 40 sasa, mtu anakuja tu na kulazimisha kununua kwa bei anayotaka hili halikubaliki kwani hakuna siku tumekaa kikao cha familia na kuteua mtu wa kufungua mirathi.”amesema
“Kinachotuhuzunisha tumeenda kumuona Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi William Lukuvi lakini hajatusikiliza bali alituambia hawezi kufanya lolote kwa sababu tumekuwa tukifungua kesi na kushindwa. Amesema.
Kwa upande wa Mjane Amina Mrisho amemuomba Rais Samia kuunda tume ya uchunguzi katika sakata hilo kwa kuwa hata maamuzi ya Mahakama yamekuwa yakipuuzwa kwani wakati kesi inaendelea inakuja notisi jambo ambalo sio sahihi.
“Rais wetu tunakukimbilia wewe baada ya kukosa msaada katika mamlaka husika ambazo zimeziba masikio na macho ili kutimiza azma yao ya dhuluma kwa makusudi.
“Eneo hili lina tahamani ya kubwa kwani 2006 lilikuwa na thamani ya Sh. 5,4 bilioni kwa nini liuzwe Sh 2.5 bilioni, mbaya zaidi baada ya hicho kinachodaiwa kuuzwa mgawaji wa fedha alikuwa Kampuni ya Udalali ya Tambaza ndiye aligawa fedha kwa wanafamilia aliowarubuni wakiongozwa na msaliti Sophia.” Amesema
Habari Mseto ilimpomtafuta Kamishina wa Ardhi Dar es Salaam Idrisa Kayera simu yake iliita bila majibu huku kwa Upande wa Waziri Lukuvi mara zote tulimpomtafuta alikuwa anatumika.




No comments:
Post a Comment