Mkurugenzi Mtendaji wa Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi (WCF), Dkt. John Mduma, akizungumza na waandishi wa habari.
Hussein Ndubikile, Dar es Salaam
Mfuko
wa Fidia kwa Wafanyakazi (WCF) umesema waajiri wa Sekta Tanzania
wamepunguziwa kiwango cha mchango wa wafanyakazi cha mapato ya waajiriwa
wao kutoka asilimia 1 hadi asilimia 0.6 huku ukibainisha punguzo la
kiwango hicho linaanza kutumika kwa michango ya mwezi Julai mwaka huu.
Akizungumza
na wanahabari leo jijini Dar es Salaam Mkurugenzi Mtendaji wa Mfuko
huo, Dkt. John Mduma amesema mabadiliko ya punguzo hilo yamekuja baada
ya Bunge la Bajeti la mwaka 2021/22 kuweka bayana ya upunguzaji wa tozo
ikiwa utekelezaji wa Blueprint na kwamba madiliko hayo yapo kwa mujibu
wa Tangazo la Serikali namba 496G la juni 30 mwaka huu lililotolewa
dhamana na waziri husika Jenista Mhagama.
Amebainisha
kuwa licha ya punguzo la tozo la uchangiaji katika mfuko huo waajiriwa
wa sekta binafsi wataendelea mafao ya fidia kama ilivyokuwa awali kwa
mujibu wa sheria ya fidia kwa wafanyakazi na kanuni zake za mwaka 2016.
Amesisitiza
kuwa punguzo hilo ni utekelezaji wa Ilani ya Chama cha Mapinduzi
inayoelekeza mfuko kuboresha mazingira ya biashara na ufanyaji kazi wa
sekta binafsi jkwa kuiwekea mazingira rafiki.
Ameongeza
kuwa punguzo hilo litakuwa na mchango mkubwa kwa sekta hiyo ikiwemo
kupunguza gharama za uendeshaji za waajiri, kuboresha mazingira ya
ufanyaji biashara na uwekezaji nchini na kuboresha na kuimarisha
mahusiano mazuri kati ya waajiri na WCF.
Amekipongeza
Chama cha Waajiri nchini (ATE) kwa mchango mkubwa katika uboreshaji
wa huduma za waajiri na kushughulikia masuala ya mbalimabli yahayohusu
waajiri na waajiriwa likiwemo suala la tozo huku
Dkt.
Mduma amesema WCF inamshukuru Rais Samia Suluhu Hassan kwa maamuzi ya
kupunguza tozo kwa waajiri wa sekta binafsi na kulipongeza Shirikisho
la Vyama vya Wafanyakazi (TUCTA) kuwa mstari mbele kuhakikisha waajiri
wanafanya kazi wakiwa na uhakika wa kingaz za mwili.
Aidha,
amesema mfuko huo una thamani ya Sh Bilioni 437 na kwamba katika
kipindi cha miaka mitano umeendelea kukua hivyo ndani ya miaka 30
utabaki kuwa endelevu.
Kwa upande wake
Mkurugenzi wa Uendeshaji wa WCF, Anselimu Peter amesema mfuko huo un
idadi ya wanachama 24,952 na kusisitiza tathmini zinaonyesha kuwa
utaendelea kuwa imara kama waajiri wataendelea kuzingatia uchangiaji wa
michango ya waajiriwa wao.
Naye Mkurugenzi wa
Huduma za Tiba na Tathmini Dkt. Abdulsalaam Omar amesema sekta ya umma
huchangia asilimia 0.5 kwa waajiri huku sekta binafsi ikichangia 0.6 na
kwamba shughuli za sekta ziko za katika hali hatarishi ukilinganisha na
umma.
No comments:
Post a Comment