Waziri wa Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Faustine Ndungulile (wapili kulia)akipata
maelezo kutoka kwa Mkurugenzi wa Benki ya CRDB, Abdulmajid Nsekela kuhusu
huduma za CRDB Wakala kupitia Shirika la Posta. Wakwanza kulia ni Mkurugenzi wa Mawasiliano
Wizara ya Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Clarence Ichwekeleza.
Hussein Ndubikile, Dar es Salaam
Serikali
imepongeza mashirikiano ya Ubia yaliyoingiwa kati ya Shirika la Posta
Tanzania na Benki ya CRDB huku ikibainisha kupitia Mpango wa Tatu wa
Maendeleo ya Miaka Mitano imejipanga kuhakikisha wananchi wanapata
huduma za kifedha kwa njia za mifumo ya kidijitali ili kupuguza
msongamano katika ofisi za taaasisi za umma na binafsi nchi nzima
Hayo
yamesemwa leo jijini Dar es Salaam na Waziri wa Mawasiliano na
Teknolojia ya Habari , Dkt. Faustine Ndungulile katika Uzinduzi wa
Huduma za CRDB Wakala Katika Ofisi za Shirika hilo.
Amesema
takwimu za Ripoti ya Ujumuishi wa Fedha ya Finscope inaonyesha
asilimia 16.7 ya Watanzania wote wanatumia huduma za benki kidijitali,
huku asilimia 28 hawana huduma za kidijitali hivyo asilimia 35 ya watu
wanatakiwa kurasimishwa katika mifumo ya kidijitali.
"Nawapongezeni Posta na CRDB kwa ushirikiano wenu mnaonyesha wazi
mmepania kuendelea kupanua wigo wa utoaji huduma kwa pamoja nawaomba
mjitahidi muwafikie Watanzania wote," amesema Dkt. Ndungulile.
Amebainisha
kuwa tayari Serikali imeshaanza kufanyia kazi mifumo hiyo katika mikoa
ya Dar es Salaamn na Dodoma lengo likiwa kuhakikisha wananchi wanapata
huduma za malipo bima ya afya, pensheni, malipo ya bili za maji, umeme,
pamoja na malipo ya usajili wa kampuni kwa njia za kidijitali.
Amesisitiza
kuwa Serikali imeshatenga Sh Bilioni 300 kwa ajili ya Mradi wa Tnzania
ya Kidijitali na kwamba kupitia Mradi wa Anuani ya Makazi na Postikodi
itahakikisha kila eneo lina namba mizigo na vifurushi inafika kwa wakati
maeneo husika.
Ametoa rai kwa Mameneja wa
Mikoa wa shirika hilo kuutumia viizuri ushirikiano kwa kufanya kazi kwa
ufanisi pamoja na kutoa huduma bora kwa wateja kwani kutasaidia kuongeza
idadi ya watu wanaotumia za CRDB na Posta kwa mifumo ya kdijitali.
Kwa
upande wake Kaimu Postamata Mkuu, Macrice Mbodo amesema shirika hilo
limefaidika na wizara hiyo kwani huduma za Serikali ikiwemo leseni y
audereva, biashara na vyeti vitolewa na posta, serikali kuanzisha duka
la mtandao ambapo ununuzi na uuzaji wa bidhaa hufanyika kupita mtandao
pamoja utoaji wa huduma za posta kupita simu za mikononi..
Naye
Mkuurugenzi Mtendaji wa Benki hiyo, Abdulmajid Nsekela amesema CRDB
itafungua matawi zaidi 200 na kwamba ilianza na mawakala 200 kwa sasa
ina zaidi 20,000 huku akisisitiza mawakala wapya watapewa elimu wawe na
weledi kutoa huduma bora.
Nsekela amesema CRDB
imeamua kuwekeza katika teknolojia ya kidijitali ili kuweza
kuwarahishia na kuwafikia wateja wao nchi nzima pamoja kuongeza watu
wanaotumia mifumo ya kidijitali.
Mkuu wa
Kitengo cha Uwakala na Usambazaji wa benki hiyo, Erick Wille amesema
kupitia ushirikiano huo pande zote mbili zitaongeza ufanisi pamoja na
kuongeza ajira 250 nchi nzima.
Erick amefafanua
huduma zitakazopatikana ni ufunguzi wa akaunti, namba za NIDA, Huduma
za kutoa na kuweka pesa, malipo ya ada, tozo za Serkali za taasisi zaidi
ya 200, manunuzi, bima pamoja na malipo ya bili z umeme na maji.
Meneja
Mkuu Uendeshaji wa Biashara wa Shirika la Posta Constantine Kasese
amesema shirika hilo lina Ofisi 67,000 duniani kote huku likiwekeza
katika majengo 167 ya biashara na makazi.
No comments:
Post a Comment