Waziri wa Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Dkt.
Faustine Ndungulile.
Hussein Ndubikile, Dar es Salaam
Serikali
imewaagiza Mameneja wote wa Mikoa wa Shirika la Posta Nchini
kuhakikisha wanakuwa wabunifu katika utendaji wao wa kazi ili kuzalisha
fedha za kuendesha huduma pamoja kulipa mshahara wa Mkurugenzi wa
shirika hilo huku ikibainisha watakaoishindwa hawatafaa kuwa katika
nafasi hiyo.
Maagizo hayo yametolewa leo jijini
Dar es Salaam na Waziri wa Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Dkt.
Faustine Ndungulile katika Kikao Maalum cha Viongozi wa Posta cha
Kutathimini mwaka uliopita na kupanga mikakati ijayo.
Amesema
mameneja hao wanatakiwa kuwa wabunifu katika utendaji kazi wa kila siku
lengo likiwa kutimiza malengo waliyowekewewa kusaidia uendeshaji wa
shirika na ulipaji wa mtendaji mkuu wa Posta,
"
Nendeni mkawe wabunifu matafute masoko ya bidhaa zenu timizeni malengo
mliyojiwekea mkifaulu mtaweza kuendesha shirika na kulipa mshahara wa
mkuu wenu mkishindwa hamtoshi kuwa hapo," amesema Dkt. Ndungulile.
Amebainisha
kuwa mameneja wanatakiwa kusimamia utoaji huduma kwa wateja bila
urasimu hasahasa wanapofanya kazi na taasisi binafsi pamoja na kuwapa
mafunzo watoa huduma wa shirika hilo ili kuendana na kasi ya mifumo ya
uendeshaji ya kidijitali.
Amewasisitiza
mameneja na watendaji wa shirika hilo kubuni vyanzo vipya mapato
vitakavyosaidia kuendesha shirika pamoja na kujenga utamaduni wa
kujadiliana na vyama vya wafanyakazi ili kuondoa migogoro ndani ya
Posta.
Ameongeza kuwa ifikapo mwezi Septemba
mwaka Posta na Shirika la Mawasiliano Tanzania (TTCL) wawe wamefikia
muafaka katika mgawanyo wa mali na kutangaza katika gazeti la Serikali.
Kwa
upande wake Kaimu Mkuu PostaMasta wa shirika hilo, Macrice Mbodo
amesema kikao hicho siku tano kitahusisha utoaji wa mafunzo kwa
viongozi, kupata uzoefu wa pamoja kutoka taasisi iliyofanikiwa,
kufundishwa itifaki na ustaarabu wa viongozi kutoka Chuo cha Diplomasia,
kujadili tathimini ya mwaka uliopita na changamoto, kupata mafunzo ya
kupanga malengo kutoka ofisi ya utumishi pamoja na kupata nasaha za
wakongwe wenye uzoefu wa kiposta na nje ya posta.
Naye
Mkurugenzi Mkuu wa TTCL, Waziri Kindamba amewaomba mameneja kusimamia
vyema mikoa yao kutoa ushirkiano kwa Kaimu huyo ili kuhakikisha Posta
inafikia malengo iliyojiwekea kufikia hatua ya utoaji huduma kimataifa
kwa mifumo ya kidijitali.
Mwakilishi wa
Mkurugenzi wa Mamlaka ya Mawasiliano Nchini (TCRA) Haroun Lemanya
ameishauri menejimenti ya Posta kujifunza kwa njia ya mafunzo wafikie
kutambulika viwango vya ubora wa kimataifa.
Mkurugenzi
wa Mfuko wa Mawasiliano kwa Wote Jastina Mashimba amesema mameneja hao
wampe ushirkiano Mbodo ili wafikie viwango vya utendaji kazi wa
mashirika ya kimataifa ya huduma za posta likiwemo la DHL kutoka
Ujerumani.
Mkurugenzi wa Idara ya Mawasiliano
wa wizara hiyo Mhandisi Clarence Chikweleza amewahimiza watendaji wa
shirika hilo kuendelea kufanya kiufanisi kufikia malengo waliyojiwekea
na kuwasisitiza kutoa ushirikiano kwa Waziri Dkt. Ndungulile.
No comments:
Post a Comment