Kaimu Mtendaji wa Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA), Matiko Mniko akizungmza na wanahabari leo jijini Dar es Salaam kuhusu Mkutano Mkuu wa Sekta ya Sanaa Tanzania utakaofanyika jijini humo Septemba 29 mwaka huu.
Rais
wa Shirikisho la Sanaa za Ufundi nchini Adrian Nyamangalle akizungumza
na vyombo ya habari leo jijini Dar es Salaam kuhusiana na mkutano huo
utakaofanyika Septemba 29 mwaka huu.
Rais wa Shirikisho la Muziki Tanzania, Mzee Yusuf akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam kuhusu ushiriki wa shirikisho hilo katika mkutano huo utakaofanyika Septemba 29 mwaka huu.
Rais wa Shirikisho
la Sanaa za Maonesho Tanzania, Cynthia Henjewele akizungumza na
wanahabari leo jijini Dar es Salaam kuhusu Mkutano Mkuu wa Sekta ya
Sanaa utakaofanyika katika Ukumbi wa Makumbusho ya Taifa Septemba 29,
Dar es Salaam.
Na Hussein Ndubikile, Dar es Salaam
Baraza
la Sanaa la Taifa (BASATA) kwa kushirikiana na Mashirikisho ya Sanaa
nchini linatarajia kufanya Mkutano Mkuu wa Sekta ya Sanaa Tanzania
utakaofanyika Septemba 29 mwaka huu katika Ukumbi wa Makumbusho ya
Taifa, jijini Dar es Salaam.
Hayo yamesemwa leo
jijini humo na Kaimu Mtendaji wa Baraza hilo Matiko Mniko wakati
akizungumza na wanahabari kuelekea mkutano huo ambao hufanyika kila
mwaka ukiwashirikisha wadau mbalimbali wa sanaa.
Amesema
kuwa lengo la mkutano huo ni kujadili masuala mbalimbali yahusuyo sekta
ya sanaa na kwamba ni jukwaa muhimu litakalosaidia kuboresha tasnia
hiyo kuifanya iwe rasmi na kuendeshwa kibiashara.
"
Lengo kuu la Serikali ni kuifanya sanaa iwe rasmi iendeshwe kibiashara
tutajadili mambo mbalimbali zikiwemo changamoto zinazoikabili tasnia ya
sanaa pamoja na yatakayofanikisha kazi zao kutambulika," amesema Mniko.
Amebainisha
kuwa Serikali ya Awamu ya Sita inatambua mchango wa sanaa kwani
imeanzisha Mfuko Maalum wa Sanaa ukitengewa Sh Bilioni 1 zitakazotumika
katika kutoa mafunzo na kutoa mikopo kwa wasanii wa tasnia mbalimbali.
Amesisitiza
kuwa mkutano huo umebeba kauli mbiu isemayo Sanaa Biashara huku
akiongeza utahudhuriwa na wataalamu kutoka vyuoni na wafanyabiashara wa
tasnia hiyo hivyo amewaomba wasanii na wananchi kuhudhuria kutoa maoni
na mapendekezo yatakayosaidia kuboresha sekta ya sanaa nchini.
kwa
upande wake, Rais Shirikisho la Muziki Nchini ambaye pia ni muimbaji wa
muziki wa Taarab, Mzee Yusuph amesema mkutano huo utasaidia kutoa
majibu ya maswali wanayoulizana wasanii hivyo amewahimiza kuchangamkia
fursa hiyo na kuacha kuongea mitandaoni badala wahudhurie ili wachangie
mawazo yatakayoleta tija kwenye tasnia ya sanaa.
Nae,
Rais wa Shirikisho la Filamu Tanzania, Elia Mjata ameipongeza
kulishukuru BASATA kwa kuwashirikisha kuhudhuria mkutano huo na kwamba
wasanii wajikoteze kujadili na kutatua changamoto lengo ikiwa kuifanya
sanaa iwe biashara.
Rais wa Shirikisho la Sanaa
za Ufundi, Adrian Nyamangalle amefafanua kuwa mkutano huo utasaidia
kubadilisha mtazamo hasi waliyonayo watu kuwa sanaa ni anasa na badala
yake utawafanya watambue kuwa sanaa ni burudani, ajira na biashara.
Rais
wa Shirikisho la Sanaa za Maonesho Tanzania, Cynthia Henjewele amesema
mkutano huo utaleta tija kwa kujadili changamoto zinazoikabili sanaa
ikiwemo sanaa hizo na kuwajenga wasanii kuifanya kua biashara.
No comments:
Post a Comment