HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

September 17, 2021

Equity Bank yazindua Huduma Ya Miamala ya Fedha za Kigeni Kupitia EazzyFX


 
Equity Bank leo hii imezindua huduma yake mpya ya EazzyFX itakayomuwezesha mteja kununua na kuuza fedha za kigeni kwa njia ya mtandao pasipo kufika benki au vituo vya kubadilisha fedha. Jijini Dar es Salaam
 
Akizungumza na waandishi wa habari katika hafla ya uzinduzi rasmi wa huduma hiyo, jijini Dar es Salaam, Mkurugenzi Mkuu wa benki ya Equity Robert Kiboti amesema kuwa huduma hiyo itarahisha huduma ya ‘Forex’ na itaondoa ulazima wa wateja kufika benki kila watakapo badilisha fedha za kigeni.

Mkuu wa kitengo cha hazina Raymond Njuu amesema kuwa huduma hiyo ni rahisi, salama na itapunguza muda ambao wateja walikuwa wanatumia kuwasiliana na benki, au kwa kutumia barua pepe au kwa njia ya ana kwa ana. 

 
Pia, Njuu amesema kuwa sasa huduma za kibenki zime hararishwa kutoka benki kuwa sehemu ambayo mteja anakwenda kwenye huduma ambayo mtu anaweza kuipata popote pale alipo na kuongeza kuwa mteja atatakiwa kuingia ndani ya tovuti ya EazzyFX mtandaoni na ataweza kufurahia huduma hio katika siku 5 za kazi kila wiki kuanzia saa 3 asubuhi hadi saa 11 jioni.

Aidha, watumiaji wa huduma hiyo wataweza kufanya miamala ya fedha hizo za kigeni kwa kuangalia viwango vya kubadilisha fedha duniani na hii itarahisisha mambo mbalimbali kama vile manunuzi ya bidhaa kutoka nchi za kigeni, ulipaji wa bili na huduma zingine.

Benki ya Equity inakuwa benki ya kwanza kutoka nchini Tanzania kuleta huduma hii ya miamala ya fedha za kigeni kwa njia ya mtandao na kuwaasa wateja kuchangamkia fursa hio kwani ni rahisi na ni ya haraka zaidi. 

 



No comments:

Post a Comment

Pages