Mmoja wa wanufaika wa mpango wa kuwajengea uwezo kutoka Manispaa ya Moshi, Elibahati Kimaro.
Mmoja wa wanufaika kutoka Hospitali ya Benjamin Mkapa, Dk. Anthony Gyunda.
Na Mwandishi Wetu
Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Joyce Ndalichako ameongoza hafla ya ushirikiano wa Tanzania na India Katika masuala ya Teknolojia na Uchumi katika Ubalozi wa India nchini Tanzania.
Hafla hiyo ilifanyika jioni ya Jana ambapo Waziri Ndalichako alikuwa Mgeni rasmi wa tukio Hilo.
Akizungumza katika hafla hiyo Waziri Ndalichako alisema mashirikiano yaliyopo baina ya Serikali hizo mbili yataendelezwa Ili kuenzi undugu na urafiki wa mataifa hayo.
"Kwa niaba ya wizara ya Elimu na Teknolojia na Kwa niaba ya Serikali na Wananchi wa Tanzania napenda kuchukua nafasi hii kutoa shukrani za dhati Kwa ushirikiano mkubwa uliopo kati ya Tanzania na India na hasa katika masuala ya Uchumi na Teknolojia.
"Nchi zetu hizi mbili zimekuwa zikishirikiana katika mambo mengi katika kuhakikisha kwamba runajenga Nguvu kazi yenye weledi. Lakini pia tumekuwa tukishirikiana zaidi katika masuala ya teknolojia na katika uanzishwaji wa viwanda vidogo, vya kati na viwanda vikubwa." alisema na kubainisha kuwa.
"Serikali ya India imekuwa ikiisaidia Serikali ya Tanzania katika kuhakikisha kwamba hizi nchi mbili zinaendeleza uhusiano mkubwa ambao uliasisiwa na waasisi wa mataifa haya mawili ambapo uliasisiwa na Hayati Mwalimu Julius Kambarage Nyerere na Waziri Mkuu wa India ambao Kwa pamoja walikuwa na urafiki wao' binafsi lakini wakaunganisha mataifa haya ambapo hadi leo tunafurahia.
"Tanzania kupitia huu mkakati wa masuala ya teknolojia na uchumi tumeweza kupeleka wanafunzi wengi India kwenda kusoma ambapo tulianza mwaka 2012 na wanafunzi 24 lakini idadi hiyo imekuwa ikiongezeka." Hata hivyo Ndalichako aliongeza kuwa.
"Wanufaika wanaonufaika na mafunzo ni watumishi katika taasisi za kawaida pamoja na watu ambao wanahusika na masuala ya kisiasa. Kupitia ushirikiano wa Tanzania na India tumeweza kuanzisha mafunzo ya tehama ya hali ya juu ya taasisi yetu ya Mbeya pamoja na taasisi ya teknolojia ya Dar es Salaam.
"Lakini kupitia ushirikiano huu tumeweza kuleta walimu kusoma na kuimarisha ujuzi wao na mafunzo ya tehama na watu ambao wameenda kupata mafunzo na kuyatoa Kwa lugha yetu ambapo yataongeza uwezo kwa wahadhili wetu ambayo yanawezesha nchi kuweza kupiga hatua kupitia ushirikiano huo."alisema
Waziri Ndalichako alisisitiza kuwa Serikali ya Tanzania itaendelea kushirikiana na Serikali ya India ikiwa ni kuenzi na kuendeleza mashirikiano wa Viongozi waasisi wa ushirikiano huo.
No comments:
Post a Comment