Na Mwandishi Wetu
TAASISI ya Elimu Tanzania imekabidhi jumla ya vitabu 173,990 kwa ajili ya shule za Msingi na vitabu 2,714 kwa ajili ya shule za Sekondari, katika wilaya ya Muleba mkoani Kagera.
Mkuu wa Wilaya ya Muleba Toba Nguvila, amesema kwamba vitabu hivyo itaondoa upungufu wa vitabu kwa wanafunzi wilayani humo.
Akizungumza wakati wa mapokezi ya vitabu hivyo Nguvila amemuagiza Mkurugenzi Mtendaji, Maofisa Elimu na walimu wote kuhakikisha vitabu vinatumika ipsavyo kama ilivyokusudiwa na serikali katika kuhakikisha wanafunzi wanapata vitabu vya kutosha kufikia lengo la elimu bora.
"Tunataka wilaya ya Muleba iwe kinara wa elimu kwa maana ya ufaulu, kuongoza kitaifa na inawezekana kwasababu tayari Mhe. Rais ametupa vitabu kupitia Taasisi ya Elimu Tanzania na nina amini vitabu hivi vinaenda kutumika kama vilivyokusudiwa," amesema Nguvila.
Ofisa Elimu wa shule za msingi, Mwalimu Severine Musyangi amesema vitabu hivyo vitasaidia kupunguza uhaba ulikuwepo wa vitabu kwa wanafunzi.
Amesema kwa sasa ujio wa vitabu hivyo utawezesha wanafunzi kupata kitabu kimoja kwa kila mwanafunzi.
No comments:
Post a Comment