Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya Tips Forum, Nancy Matta akizungumza na wanahabari leo jijini Dar es Salaam kuhusu Mashindano ya Miss Tanzania Eastern Zone yatakayofanyika mkoani Morogoro Septemba mwaka huu.
Hussein Ndubikile, Dar es Salaam
Warembo
16 wanatarajiwa kushiriki Fainali ya Mashindano ya Urembo ya Kanda ya
Mashariki 'Miss Tanzania Eastern Zone' yatakayofanyika katika Hoteli ya
Morena mkoani Morogoro Septemba 24 mwaka huu.
Hayo
yasememwa leo jijini Dar es Salaam na Mkurugenzi wa Kampuni ya Tips
Forum ambao ndio waandaaji wa mashindano hayo ambaye pia ni Miss Mbeya
Mwaka 2018/19, Mhandisi Nancy Matta wakati akitoa taarifa ya mwelekeo
kuelekea fainali hiyo.
Amesema kuwa tayari
maandalizi ya mashindano hayo yameshakamilika na warembo kutoka mikoa ya
Lindi, Pwani, Morogoro na Mtwara wamesharipoti kambi ya Dynasty Hotel
Beach na kwamba wakiwa hapo watapatiwa huduma ya malazi na mazoezi
kutoka kwa walimu.
" Miss Tanzania Kanda ya
Mashariki jana wameripoti kambini tayari wakiwa hapa watapatiwa malazi
na mazoezi tunaamini washindi watawakilisha vyema katika Mashindano ya
Miss Tanzania ambapo mshindi ataiwakilisha katika mashindano ya dunia ya
urembo," amesema mhandisi Nancy.
Amebainisha
kuwa lengo kuandaa mashindano hayo kuendelea kuunga mkono Serikali
juhudi za kutangaza utalii wa ndani na nje hivyo anaamini warembo hao
watakuwa mabalozi wa kutangaza vivutio vya utalii watakavvyovitembelea.
Amesisitiza
kuwa mshind wa kwanza atapata kitita cha fedha taslimu Sh Milioni 2, wa
pili Sh mil 1.5 na wa tatu atazawadiwa Sh mil moja huku washiriki
waliobaki watapatiwa kila mmoja Shilingi laki moja.
Kwa
upande wake, Mwakiishi kutoka Chaneli ya Safari ambao ndio wadhamini
wakuu wa mashaindano hayo, Magreth amesema wamefarijika kuyadhamini huku
akibainisha yatakuwa chachu ya kutangaza utalii wa nchi.
Nae,
Mwakilishi kutoka Bodi ya Utalii Nchini (TTB), Maria Mafie amefafanua
kuwa warembo hao watapata fursa kutembelea Mbuga za Saadan na Nyerere
hivyo mshindi atakuwa balozi wa kutangaza utalii wa nchi kwani wana
malengo ya kuongeza idadi ya watalii kuongeza mapato.
Meneja
Masoko wa Dynasty, Niwako Charles amesema wamefurahi kuwa wadhamini wa
Miss Kanda ya Mashariki na kwamba wana jukumu la kutoa malazi kwa
warembo huku akiwakaribisha kufika hapo kujionea mazoezi yao.
Meneja
Mauzo wa Hoteli ya Serena, Shaban Kaluse amesema wameamua kuunga mkono
mashindano hayo kuhamasisha utalii wa ndani na nje kwani mshindi
ataiwakilisha nchi katika mashindano ya dunia.
Mlezi/Mwalimu
wa Warembo hao, Evangelina Peter amemshukuru mkurugenzi wa kampuni hiyo
kwa kumwamini kuwa mlezi hivyo anaamini mshindi atawaiaklisha nchi
vyema endapo atashinda taji la Miss Tanzania.
Wadhamini wengine ni Sumala Sports Morogoro, Kiwanda cha Ngozi, Dizzim FM, It's all Cards na Hoteli ya Art.
No comments:
Post a Comment