Wajumbe wapya wa bodi ya TANESCO.
Na Hussein Ndubikile, Dar es Salaam
Waziri
wa Nishati,January Makamba amesema ni wakati sasa Shirika la Umeme
Tanzania TANESCO linatakiwa kuanza kujiendesha kibiashara, kwa ufanisi
ili kuchangia uchumi wa Taifa.
Ameyasema
hayo jijini Dar es Salaam Katika Ukumbi wa kimataifa wa Mkutano wa
Mwalimu Nyerere wakati akizungumza na Mameneja wa TANESCO wa ngazi ya
Kanda, Mikoa, Wilaya na Makao Makuu.
Aidha
Waziri Makamba amewatambulisha Wajumbe wa Bodi ya TANESCO wakiongozwa
na Mwenyekiti Omari Issa, pamoja na Mkurugenzi Mtendaji Maharage Chande,
walioteuliwa Septemba 25, 2021 na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania Samia Suluhu Hassan.
Wajumbe
wa Bodi ya TANESCO waliotambulishwa ni pamoja na Nehemia Mchechu,
Zawadia Nanyaro, Lawrence Mafuru, Mhandisi Cosmas Masawe, Balozi
Mwanaidi Maajar, Mhandisi Abdallah Hashim, Abubakar Bakhresa na
Christopher Gachuma.
Mhe. Makamba amesema Bodi iliyochaguliwa ina wajumbe kutoka nyanja mbalimbali na watasaidia Shirika kufikia malengo.
"Tunataka
baada ya miaka mitatu Shirika liingie katika orodha ya mashirika bora,
yenye thamani na yanayoheshimika Afrika" alisema Mhe. January Makamba
Naye
Mwenyekiti wa Bodi ya TANESCO, Bw. Omari Issa, amesema atahakikisha
Bodi inafanya kazi na kutimiza malengo yake kwa kufuatilia kwa karibu
utekelezaji wa malengo na uwajibikaji.
Mkurugenzi
Mtendaji, Bw. Maharage Chande, ameeleza vipaumbele ambavyo ni masilahi
ya rasilimaliwatu, Wateja wa Shirika na utekelezaji wa mipango, hivyo
ameomba ushirikiano kutoka kwa wafanyakazi wa TANESCO.
"Nimhakikishie
Mhe. Waziri tutahakikisha tunarudisha heshima ya Shirika na ufanisi
kupitia ushirikiano wenu, hakuna Shirika lolote linalotoa huduma ya
umeme zaidi yetu sisi, yamkini tuwape wateja wetu huduma wanayostahili",
" alisema Bw. Maharage Chande
Meneja
Mwandamizi Rasilimaliwatu, Bw. Francis Sangunaa, aliwahakikishia
viongozi ushirikiano kwa niaba ya wafanyakazi wa TANESCO.
No comments:
Post a Comment